Na MWANDISHI WETU
-DODOMA
Serikali imeanza imeanzisha mchakato wa mazungumzo kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mto Lumpungu mkoani Kigoma.
Mto huo ambao umepita katika mpaka unatenganisha nchi za Tanzania na Burundi hivyo ujenzi wa daraja hilo lazima uhusishe nchi hizo mbili.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni leo Apri 5,2023 wakati Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali la mbunge wa Muhambwe Dk. Florence Samizi (CCM).
Kutokana na hali hiyo, Dk. Samizi ametaka kujua ni lini Serikali ya Tanzania na Burundi wataanzisha mazungumzo ya kujenga daraja la mto Lumpungu ambalo litarahisisha mawasiliano ya kibiashara kwa nchi mbili na kukuza uchumi.
Mbunge huyo amesema daraja hilo ni muhimu kwa wananchi waishio vijiji jirani kwa pande zote na akaomba mchakato ufanyike kwa haraka.
Naibu Waziri amesema Wizara ya Ujenzi ilishaliona hilo nankutambua umuhimu wake lakini wadau wanaotakiwa kushiriki ni wengi.
“Sisi Wizara ya Ujenzi tumeshajipanga lakini kazi hii inahusisha vyombo vya ulinzi, Tamisemi,Wizara ya mambo ya nje na wadau wengine, kwa hiyo hadi nao waone umuhimu wa kuwepo kwa daraja hilo,” amesema Ngonyani.
Hata hivyo amesisitiza kuwa watazishirimisha taasisi hizo ili nao waone umuhimu wa uwepo wa daraja hilo kwa ajili ya uchumi.