Home BIASHARA SMZ: Ushirikiano, mchango wa NMB kwa maendeleo ya Zanzibar ni wa kuigwa

SMZ: Ushirikiano, mchango wa NMB kwa maendeleo ya Zanzibar ni wa kuigwa

Google search engine
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah (watatu kushoto) akisalimiana na Mkaguzi mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (watatu kulia) baada ya kuwasili katika Hotel ya Golden Tulip Zanzibar kushiriki ibada ya Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa wateja wake, viongozi wa Dini na wa serikali Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Idara ya huduma za Serikali wa Benki ya NMB, wapili kulia ni meneja mwandamizi wa Idara ya Huduma za Serikali, Adelard Mang’Ombo na wanne kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar, Mahmoud Mohammed Mussa.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah (Katikati) akiteta jambo na Mkaguzi mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (wapili kushoto) na  Meneja wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame (wapili kulia) mara baada ya kushiriki ibada ya Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa wateja wake, viongozi wa Dini na wa serikali Zanzibar katika Hoteli ya Golden Tulip visiwani humo. kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mjini Magharibi, Rashid Simai Msaraka na Kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar, Mahmoud Mohammed Mussa.

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imekiri kuvutiwa na jitihada za Benki ya NMB visiwani humo, ikiwemo kutoa ushirikiano wa dhati na mchango uliotukuka katika kuchagiza maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla, huku ikitaka taasisi zaidi nchini kuiga benki hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Zanzibar, Hamza Hassan Juma kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Hemed Seleman Abdullah, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na NMB kwa ajili ya wateja wao, viongozi wa dini na aserikali, wadau na wananchi katika visiwa vya Zanzibar.

Akizingumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na zaidi ya watu 600, kwenye Ukumbi wa Golden Tulip Airport, Waziri Hamza Hassan Juma alisema kuwa,  Serikali yake inatambua,  kuthamini na kuvutiwa na kiwango cha mashirikiano baina ya NMB na SMZ katika jitihada za kukuza uchumi, kuleta maendeleo na kurahisisha vita ya kupambana na umaskini.

“Kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, napenda kufikisha kwenu salamu zake za pongezi kwa NMB kwa ushirikiano wa dhati inayotoa kwa SMZ, pamoja na inavyotoa mchango mkubwa katika kuunga mkono jitihada za kuleta maendeleo Zanzibar.

“SMZ tunatoa shukrani za dhati kwa NMB namna inavyojitoa kustawisha maendeleo ya Wazanzibar. Mabenki mengine na taasisi zingine zinapaswa kuiga kwa benki hii inavyoshirikiana na Serikali kuleta maendeleo kuunganisha nguvu za kupambana na umaskini,” alibainisha Waziri Hamza Hassan.

Kuhusiana na utamaduni chanya na endelevu wa kufuturisha wateja, wa benki hiyo Waziri huyo alisisitiza kuwa NMB inafanya jambo kubwa ambalo sio tu kiibada, bali pia linaloongeza imani kwa jamii, huku akibainisha kuwa wao kama Serikali wanaiombea kheir benki hiyo ambayo ustawi wake unabeba manufaa mapana kwa Watanzania wote.

Awali akimkaribisha Waziri Hamza Hassan,  Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, alisema kufuturisha wakati wa mwezi wa Ramadhani ni utaratibu wao wa kila mwaka, wanaoutumia kujumuika pamoja na wateja wao kutekeleza Ibada hiyo muhimu.

“Hii sio mara ya kwanza kwa NMB, tumefanya hivi kila mwaka, ambapo mwaka huu tumeanzia Dar es Salaam, leo tuko hapa Unguja, kisha tutaenda kufuturisha Pemba na baadaye jijini Dodoma,” alisema Baragomwa mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwamo Spika wa Baraza la Wawakilishi na Meya wa Zanzibar.

Baragomwa akabainisha kuwa: “Wakati wa mwezi huu, Waislamu huutumia kutafakari wema na utukufu wa Mungu, pamoja na kuzingatia maadili yanayotuunganisha binadamu. Pia huonyesha upendo kwa familia zetu, kutoa shukrani kwa Mung, kuomba toba na kudumisha ibada.

“Tunaamini ya kwamba kupitia mwezi huu, jamii zetu zinastawishwa kwa sala na dua za dhati zinazotolewa wakati huu, ambazo ni baraka kwa maisha ya wengi na Taifa kwa ujumla,” alisisitiza Baragomwa huku akiwakumbusha Waislamu kutafakari kwa kina juu ya upendo wa Mungu kwa wanadamu.

Aliongeza ya kwamba ni vema waumini wa Kiislamu wakadumisha ibada hata baada ya Mwezi wa Ramadhani, na kujikurubisha kwa Mungu wao, huku akiwaombea Wazanzibar na Watanzania wote kila la kheir katika Siku zilizo baki kukamilisha Ibada ya Funga ambayo ni Nguzo ya nne kati ya Tano za dini yao.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here