Home KIMATAIFA Putin anatumia chakula kama silaha- Yara

Putin anatumia chakula kama silaha- Yara

Google search engine

Moscow, Urusi

Vladimir Putin anatumia “chakula kama silaha”, na madhara yake yanaonekana duniani kote, bosi wa kampuni kubwa ya mbolea duniani ameonya.

Svein Tore Holsether, kutoka Yara, amesema nchi zinahitaji kupunguza utegemezi wao kwa Urusi baada ya uvamizi wake nchini Ukraine kuathiri usambazaji wa chakula na bei ya kimataifa.

Urusi ni muuzaji mkuu wa mbolea na kemikali zinazotumiwa kuzitengeneza.

Lakini vita hivyo vimesababisha masuala ya usambazaji na kuongeza bei ya gesi asilia, ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa mbolea.

Matokeo yake, bei za mbolea duniani zimefikia viwango vya juu na kuwalazimu wakulima kupandisha bei ya chakula, jambo linaloweka shinikizo kwa watumiaji duniani kote.

“Putin ametumia nguvu za kivita na anatumia chakula pia,” Holsether aliambia BBC mwanzoni mwa Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos.

“Ni msemo, ‘nidanganye mara moja, aibu. Nidanganye mara mbili, aibu juu yangu,”

Onyo hilo linarejelea wasiwasi kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Fedha . Pia akizungumza na BBC, mkurugenzi wake mkuu Kristalina Georgieva alisema dunia inapaswa “kuelekeza umakini kwenye mbolea leo, kwa sababu hapa ndipo tunapoona tishio la uzalishaji wa chakula na kwa hivyo bei ya chakula mnamo 2023”.

Aliongeza: “Bei ya mbolea inabakia kuwa juu sana. Uzalishaji wa amonia [ambayo hutumiwa kutengeneza mbolea] katika Umoja wa Ulaya, kwa mfano, ilipungua sana. Yote haya yanahusiana, bila shaka, na athari za vita vya Urusi juu ya bei ya gesi na upatikanaji wa gesi.”

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here