Google search engine
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas (wapili kushoto) akipokea makabati madogo ya kuhifadhi vitu vya wagonjwa kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini, Janeth Shango (Kulia) wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba mbali mbali kwa hospitali ya Mt. Benedicto, Ndanda. Benki ya NMB imekabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 kwa hospitali hiyo. kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Masasi, Lauter Kanoni na Wapili kulia ni Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Isaiah Michael Seinz

Na MWANDISHI WETU

-MTWARA

BENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa tiba kwa hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Benedict ya Ndanda iliyopo Wilayani Masasi mkoani Mtwara vyenye thamani ya zaidi ya Sh15 millioni. 

Vifaa hivyo ni pamoja na vitanda vitano vya kulazia wagonjwa wa kawaida pamoja na magodoro yake, mashuka 100, makabati madogo kumi, vitanda vya wagonjwa wasiojiweza vitano, viti vya magurudumu vitano, stendi za kusimamishia dripu kumi na ‘screen’ za hospitali tano. 

Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kusini, Janeth Shango alisema jana kuwa vifaa hivyo ni moja ya ushiriki wa Benki ya NMB katika maendeleo ya jamii na Benki hiyo inayo wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida inayopatikana. 

“Afya ni moja ya kipaumbele kwa Benki ya NMB na ni kutokana na ukweli kuwa afya ni msingi mkubwa sana kwa maendeleo ya Taifa lolote hapa duniani” alisema Janeth. 

Alisema Benki hiyo kama wadau wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo za serikali kwa kusaidia jamii kwani jamii ndizo zimeifanya Benki ya hiyo kuwa hapa ilipo na kubwa kuliko Benki yoyote hapa nchini.     

Katibu wa Hospitali ya Mtakatibu Benedict, Joseph Ndukusi Saiburu alisema kuwa msaada wa Benki hiyo ni muhimu na umekuja wakati muafaka ambapo hospitali hiyo inafanyiwa ukarabati. 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas (kushoto) akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kusini, Janeth Shango (Kulia) wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba mbali mbali kwa hospitali ya Mt. Benedicto, Ndanda. Benki ya NMB imekabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 kwa hospitali hiyo. Katikati ni Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Isaiah Michael Seinz

“Tumefanya ukarabati wa wodi nyingi unaoenda na kuweka vitanda vya kisasa na hivi vitanda ni gharama, msaada huu umekuja muda mzuri, tuna uhitaji wa vitanda 200 vya kisasa huu msaada umetuongezea nguvu, tuna mpango wa kununua kidogo kidogo kwa sababu ni ghali” alisema Katibu wa hospitali. 

“Hiyo pesa tutapeleka kwenye vitu vingine, tuna upungufu wa screen za hospitali (zile stendi ambazo zko pembeni ya vitanda) zinaongeza usiri kwa mgonjwa” alisema. 

Alisema Benki ya NMB imewafanyia kitu kikubwa sana kwa vifaa tiba hivyo, na kuongeza kuwa meza za kuhifadhia na kulia chakula walizopewa zitasaidia katika wodi binafsi iliyoo hospitalini hapo. 

 Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas alitoa rai kwa Benki ya NMB kuendelea kufikiria vituo vingine vya afya na hata mashule yaliyo katika uhitaji. 

Vile vile Kanali Abass aliiomba Benki ya NMB kuendelea kubuni bidhaa na huduma nafuu zaidi ambazo mfanyankazi wa kawaida anaweza kumudu na kuzidi kuboresha huduma kwa wateja hasa watumishi wa afya ili idadi yao iweze kuonegzeka jambo ambalo litawapa fursa nyingi zikiwemo kukopa ili wawe na amani wanapokuwa kazini na kuongeza tija kwenye ameneo yao kazini. 

“Nawapongeza sana NMB kwa kuchagua kutoa mchango wao wa vifaa tiba hapa hospitali ya Ndanda iliyopo wilayani Masasi mkoani hapa: alisema” Kanali Ahmed. 

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here