Google search engine
Aliyekuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

MOJA Habari kubwa ndani ya jamii ya Watanzania kwa sasa ni kuhusu uamuzi wa Baraza la Ulamaa chini ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), kuhusu uamuzi wa Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeiri Bin Ally wa Mbwana, kutangaza kutengua nafasi ya aliyekuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar e Salaam, Alhad Mussa Salum.

Ni wazi uamuzi huu huenda kuna baadhi wasiuelewe lakini mimi binafsi nimeulewa hasa kutokana na rekodi inayotia shaka ya Sheikh Alhad hasa kutokana kauli na kiburi kilichojaa ndani yake.

Umma wa Waislamu na Watanzania walio wengi hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam, walishachoka na kauli na vitimbi vyake ila tu walikuwa wakivumilia kwa kuwa mwenye nafasi ya uteuzi ni Baraza la Ulamaa la Bakwata lakini kama ingekuwa wana uamuzi wa papo kwa hapo waislamu wenyewe siku nyingi wangeshasaidia kuchukua uamuzi dhidi ya Sheikh Alhad.

Moja kati ya kumbukumbu ambayo mpaka sasa Watanzania waliowengi ni mshangao wa hatua hii kuchelewa kwani Bakwata walitakiwa kuchukua hatua tangu mwaka 2019 ambapo Alhad alikuwa na kauli tata hasa kutokana na kuwafanisha viongozi wa nchi yetu akiwamo Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Pombe Magufuli kwani ni zaidi ya Yesu au Mtume Muhammad, ambapo kwa mujibu wa wana zuoni wa dini zote (Uislamu na Ukrito) walipinga na mfano wake wake huu.

Inaweza kuwa ‘kila masika na mbu wake’ na sasa hatua ya mgogoro wa ndoa wa ‘Dk’ Juma Mwaka ndio ilikuwa mtego wa safari yake, na hii inaonyesha wazi Alhad kupingana wazi wazi na utetezi wa kundi kubwa la Waislamu ambao wanataka heshima ya Mahakama ya Kadhi kutambulika kama njia ya tiba ya migogoro ya ndoa na hata miradhi kwa jamii ya Waislamu.

Tangazo la Februari 2, 2023 usiku ya Baraza la Ulamaa ambalo lilitengua uteuzi wake na kumteua Sheikh Walid Alhad Omari Bin Kawambwa huku chanzo cha ndani kikieleza kuwa kujawa kiburi kwa Sheikh Alhad kwa kile kinachodaiwa kwamba ‘hagusiki’ kutokana na mtandao wake aliojenga ndani ya Serikali tangu awamu iliyopita.

Hakika Mungu ni mwema ndoa ya Mwaka imekuja kuwa sababu na hii inatokana na yeye kutambua haki yake kwa kuipambania kwa mamlaka za ndani ya Bakwata. Lakini swali kubwa ambalo jamii inajiuliza je ni ndoa ngapi zimeamuliwa ‘kihuni’ na wahusika wakishindwa kupaza sauti zao kwa hofu ya ‘kuminywa’.

Jeuri, majivuno ilikuwa ni hulka yake kila awapo mbele ya jamii pasi na kuangalia maslahi ya umma hasa wa Waislamu na hakika Sheikh Alhad alishapoteza sifa kabla ya kuvunja ndoa ya Dk Mwaka.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here