Home KITAIFA CHANZO AJALI ILIVYOUA WATU 17 MKOANI TANGA

CHANZO AJALI ILIVYOUA WATU 17 MKOANI TANGA

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, TANGA

WATU 17 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya magari mawili likiwemo gari iliyokuwa ikisafirisha msiba kugongana uso kwa uso usiku wa kuamkia leo Jumamosi Februari 4, 2023 katika eneo la Magira Gereza wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Imeelezwa kuwa ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar kwenda Moshi kwenye mazishi.

Akizungumzia ajali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema wananchi wa Mkoa Wa Tanga na Tanzania kwa ujumla wamepokea kwa masikitiko makubwa tukio la ajali hiyo iliyotokea usiku wa leo ikihusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 17 na majeruhi 12 pamoja na uharibufu mkubwa wa nagari hayo.

“Ajali imetokea Februari 3,2023 , saa 4.30 usiku eneo la Magila Gereza katika Kata ya Magila Gereza Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe, Barabara Kuu ya Segera – Buiko. Magari yaliyohusika na ajali hiyo ni gari namba T 673 CUC aina Mitsubish Fuso Ikiendeshwa na Dereva ambaye jina lake halijafamika iligonga na gari T 863 DXN aina ya Coaster Coaster Iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na Abiria 26 Ikiyokea Dar es Salaam kuelekea Moshi Kilimanjaro kwa mazishi.

“Ajali hii imesababisha vifo 17 na najeruhi 12 ambao majina yao wote Hayajafahamika. Miili ya narehemu imehifafhiwa katika Hospital yetu ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospital ya Mkoa wa Tanga Bombo na majeruhi 2 wamebaki Hospital ya Korogwe kwa Matibabu,”amesema Mgumba

Aidha ameeleza kwamba chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa gari namba T 673 CUC M/Fuso Kulipita gari la mbele bila ya kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso gari namba T863 DXN T/Coaster.

KAULI YA NDUGU

Mtoto wa kaka wa marehemu, Ginnes Mrema, amesema kuwa jana baada ya kumaliza ibada za kuaga mwili walianza safari ya kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkuu Wilayani Rombo katika Kijiji cha Mukara ambapo marehemu alikuwa anakwenda kuzikwa.

“Wakati tunakuja tumefika Korongwe ile gari ambayo ilikuwa na wanafamilia ikapata ajali iligonga uso kwa uso na Fusso kwa hiyo pale wakawa wamefariki ndgu zetu 14 na wale waliokuwa kwenye Fusso walikuwa watatu pamoja na mzee wetu (marehemu).

“Watoto wa marehemu ambao wamefariki yupo mtoto wake mkubwa anaitwa Nesto, mdogo wake wa kike anaitwa Agustina wote wawali wamefariki dunia na pia kwa upande wa baba yangu ambao ni baba zangu wadogo wamefariki wawili na dada yangu ambaye alikuwa na mwanaye naye amefariki palepale na wengine waliofariki kuna watoto wa baba mkubwa wengi wao ni majirani wamezunguka palepale,” amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here