Na MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA
TABIANCHI ni hali ya mabadiliko ya mazingira upande wa hali ya hewa yaani halijoto, pepo zinazovuma na mvua ambayo yanayojirudia rudia kwa muda mrefu.
Tanzania ni nchi iliyopo mashariki mwa bara la Afrika na imepakana na nchi zifuatazo: upande wa kaskazini imepakana na nchi za Kenya na Uganda, upande wa magharibi imepakana na nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, upande wa kusini kuna nchi za Zambia, Malawi na Msumbiji wakati upande wa mashariki kuna Bahari ya Hindi.
Kutokana na hali hiyo Tanzania ni miongoni mwa nchi inayokabiliwa na mabadiliko ya tabianchi kwani asilimia 1 ya pato la Taifa inatajwa kupotea kila mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi huku ikikadiriwa kuwa watu milioni 1.6 wanaoishi ukanda wa pwani watakabiliwa na changamoto ya athari za mabadiliko ya tabia nchi ifikapo mwaka 2030.
Hata hiyo inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2030 wastani wa asilimia 2 ya pato la taifa itapotea.
Kwa sasa Tabianchi ya nchini Tanzania hubadilika kwa nyakati tofautitofauti katika mwaka.
Kutokana na hali hiyo Tanzania hupata majira ya joto katika miezi ya Desemba, Januari na Februari. Hata hivyo kiasi cha joto ni cha juu katika ukanda wa Pwani kuliko katika sehemu za Nyanda za Juu na milimani. Mbapo katika miezi hii jua la utosini huwa kwenye kizio cha kusini, hivyo Tanzania hupata joto zaidi.
Katika miezi ya Juni, Julai na Agosti, kuna hali ya baridi kwa sababu wakati huu jua la utosini huwa katika kizio cha kaskazini.
Mvua za vuli hunyesha katika miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba na mvua za masika hunyesha katika miezi ya Machi, Aprili na Mei ingawa zipo tofauti ndogo kati ya sehemu mbalimbali.
Hivyo kiasi cha mvua na halijoto husababisha tofauti za aina ya uoto wa asili, udongo na aina ya mazao yanayolimwa.
Tunajua wazi kwamba mabadiliko ya tabianchi duniani kote yanajitokeza Tanzania pia. Kwa mfano, ongezeko la joto Duniani linasababisha barafuto la mlima Kilimanjaro kuzidi kuyeyuka. Serikali ya nchi imeungana na zile za nchi nyingi kukabili tatizo hilo lakini Kigezo kikitajwa kila mara bajeti iliyopangwa ni ndogo.
Hata hivyo suala la ongezeko la gesi ukaa kwa kiwango kikubwa kumesababishwa na shughuli za kibinadamu ,
hivi karibuni uchunguzi wa kisayansi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi umependekeza kuwa kusitisha ongezeko la gesi ukaa peke yake haitasaidia kukabiliana na ongezeko la joto kufikia nyuzi joto 1.5 au 2.
Inaelezwa kuwa visiwa vya Pemba na Mombasa katika hatari ya kuangamia, ambapo majadiliano ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, yote mara zote hulenga kukabiliana na gesi ukaa ili kupunguza ongezeko la joto kabla ya mwisho wa karne hii.
Mawazo haya ambayo yamekuwa yanakanganya huku wengine wanaona kama yanaingilia ukuaji wa kibiashara.
Lakini utafiti mpya kutoka kwa wanasayansi nchini Marekani,wahandisi na wataalamu wa afya umesema kwamba kuna baadhi ya njia za tekinolojia ambazo sio nzuri na ziko tayari kutumika kwa kiwango kikubwa.
Ripoti hiyo inasema kwamba kuna fursa nyingi ambazo zinaweza kujitokeza kama gesi ukaa itaongezeka katika mimea na masalia katika ardhi iliyo kame au ufukweni na kando ya mito.
Kwa pamoja ardhi ya namna hiyo huwa inahifadhi kiwango kikubwa cha gesi ukaa katika mazingira yeyote.
Baadhi ya maeneo ya ufukweni ni miongoni mwa sehemu ya dunia ambayo imekuwa ikiathirika kila mwaka kwa hekari 340,000 mpaka 980,000.
Matatizo mengine ambayo yanaweza kujitokeza katika maeneo ya bahari duniani kote yanaweza kuharibu mazingira.
Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali, ikiwamo mitandao ya mazingira