Na MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM
VIONGOZI wa Vyama vya siasa nchini wameaswa kushirikiana ili waweze kujenga mazingira mazuri ya kufanya siasa zenye tija na siasa za kushindana kwa hoja.
Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Profesa Ibrahim Lipumba leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua Jukwaa la Majadiliano Wilaya ya Ilala kwa lengo la kuwaunganisha viongozi wa vyama vya Siasa katika wilaya hiyo kwaajili ya kuanza majadilia ya pamoja katika kuunda mshikamano na umoja.
Amesema Jukwaa hilo litawezesha majadiliano na jinsi ya kuendeleza Demokrasia, Amani na kuendeleza maendeleo ya taifa kwa Ujumla.
“Kitaifa tunajukwaa la vyama, tunakutana na viongozi wa Vyama vya Siasa kwa ngazi ya Wilaya ili kuendeleza Demokrasia na kuweza kubadilishana mawazo ni namna gani ya kuendeleza Demokrasia na kuweza kujadiliana namna ambavyo shughuli zetu za kisiasa tunazifanya kwa mujibu wa taratibu na sharia na kwaamani.” Ameeleza Prof. Lipumba
Katika jukwaa hilo wamesisistiza kwamba mambo ya msingi hasa kuwepo ni kuwa na tume huru ya uchaguzi, nimhimu ili tuweze kuwa na amani endelevu.
“Kama nchi na taifa tunahitaji kujadiliana ili tuweze kuapata tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwa na uwezo wa kusimamia chaguzi za serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025.” Ameeleza Prof. Lipumba
Amesema hayo ndio mambo ya kitaifa na jukumu la Serikali katika hatua ya Wilaya, tunahitaji viongozi wetu wa vyama waweze kushirikiana kujenga mazingira mazuri ya kufanya siasa zenye tija, siasa za kushindana kwa hoja.
Pia Prof. Lipumba amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuwa na maridhiano ya majadiliano na vyama vya siasa nchini ikiwa ni pamoja na kuruhusu vyama vya Siasa Nchini vifanye kazi zake kwa uhuru na Amani.
Amesema Rais Dkt. Samia ameruhusu Mambo mamne katika utekelezaji wa kazi za vyama vya siasa katika vipengele vine ambavyo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Ujenzi mpya wa Taifa.
Kwa Upande wa Msaidizi wa Masuala ya Siasa na Uchumi, Ubalozi wa Marekani, Bion Bliss amesema kuwa Marekani inashirikiana na washirika wake katika kuhakikisha demokrasi inaimarika, wanachi wanakauli na kuweza kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi huru, Amani, haki na uaminifu.
Amesema jukuwaa hili litawanguanisha Viongozi wa vyama vya siasa ili kuweza kuafanya siasa,Kuwa na vipaumbele vya pamoja ikiwemwo mazungumzo ya pamoja ili kuleta uelewa wa pamoja kwa wananchini wake.
Akizungumzia kuhusiana na majadiliano ya pamoja na viongozi wa vyama vya siasa, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa Jukwa hilo litakuwa eneo mhimu la kuwaweka pamoja viongozi wa vyama vya siasa ili kujadiliana changamoto mbalimbali na kuweza kupata majawabu wakiwa Mezani.
“Naamini kwamba Chini ya Uongozi wa TCD chini ya Mwenyekiti wake, Abraham Kinana na Makamu Mwenyekiti, Prof. Lipumba nchi hii itakaa kwenye meza ya majadiliano ya pamoja, tuwaombee kuelekea kwenye maridhiano na majadiliano.” Amesema Zitto