Home KIMATAIFA POLISI UINGEREZA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA MAKOSA YA UBAKAJI

POLISI UINGEREZA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA MAKOSA YA UBAKAJI

Google search engine

-BBC

JAJI wa Uingereza amemhukumu afisa wa zamani wa polisi kifungo cha maisha jela, kwa muda usiopungua miaka 30, kwa makosa kadhaa ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono kesi ambazo zimeaibisha Jeshi la Polisi la Metropolitan London.

Jaji Bobbie Cheema-Grubb alimhukumu David Carrick miaka 36 ya kifungo cha maisha kutokana na msururu wa makosa 71 ya uyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake 12.

Alisema Carrick, ambaye uhalifu wake ulijumuisha makosa ya ubakaji 48, uliwakilisha “hatari kubwa kwa wanawake” ambazo ” zitadumu kwa muda usiojulikana”.

Carrick mwenye umri wa miaka 48 ambaye alikuwa afisa wa polisi wa muda mrefu wa Met, jeshi kubwa la polisi la Uingereza, atatumikia miongo mitatu gerezani kabla ya kuzingatiwa kwa msamaha.

Jeshi hilo limeapa kukomesha utamaduni wa chuki dhidi ya wanawake na uzembe ulioangaziwa na ubakaji na mauaji ya msichana ambaye alikamatwa barabarani na afisa wa polisi mnamo Machi 2021.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here