Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza hali ya hatari ya miezi mitatu katika mikoa 10 iliyoathiriwa zaidi na tetemeko la ardhi ambalo limesababisha vifo vya maelfu ya watu.
Bw Erdogan alisema kuwa idadi ya vifo nchini Uturuki imeongezeka hadi watu 3,549. Zaidi ya watu 1,600 wanaripotiwa kufariki nchini Syria.
Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Erdogan alisema hali ya hatari imewekwa ili kuhakikisha kazi ya uokoaji inaweza “kufanywa haraka” kusini-mashariki mwa nchi.
Alisema hatua hizo zitaruhusu wafanyikazi wa misaada na misaada ya kifedha kufika kwa urahisi katika mikoa iliyoathiriwa, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Hali ya hatari itaondolewa kabla ya uchaguzi wa Mei 14, wakati Erdogan atakakuwa akipojaribu kutafuta rudhaa ya kusalia mamlakani baada ya miaka 20.
Mara ya mwisho Uturuki ilitangaza hali ya hatari ilikuwa mwaka 2016 baada ya jaribio la mapinduzi lililotibuka. Iliondolewa miaka miwili baadaye