Home KITAIFA MBOLEA YA RUZUKU YAPUNGUZA GHARAMA ZA UZALISHAJI ZAO LA KAHAWA NCHINI

MBOLEA YA RUZUKU YAPUNGUZA GHARAMA ZA UZALISHAJI ZAO LA KAHAWA NCHINI

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA

IMEELEZWA kuwa mpango wa mbolea ya ruzuku umeleta nafuu kubwa kwenye shughuli  za uzalishaji wa  kahawa kwa kampuni ya kilimo cha kahawa ya Karatu Coffee Eatate LTD iliyoko Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Kabla ya serikali kuja na mpango wa mbolea ya ruzuku kampuni ilikuwa ikitumia kiasi cha Sh milioni 250 hadi 300 kwa ajili ya mbolea lakini kwa masimu wa kilimo 2022/2023 kiasi cha Sh milioni 120 hadi 140 kimetumika na kutoa nafuu kubwa kwenye uzalishaji.

Hayo yameelezwa na Meneja wa shamba hilo, Ladislaus  Kauku alipofanya mahojiano na wanahabari kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania shamabni kwake, mahojiano yaliyolenga kujua manufaa aliyopata kutokana na uwepo wa mbolea za ruzuku.

Kauku alieleza kuwa, mpaka sasa wamenunua mifuko 1400 ya mbolea za ruzuku mifuko 700 mbolea ya Urea na mifuko mingine 700 ya mbolea aina ya NPK.

 Alieleza kuwa  wameshaweka mbolea ya majani tunasubiri awamu aina ya NPK kwa ajili ya majani wanasubiri mvua inyeshe ili waweke mbolea awamu ya pili kwa ajili ya mbegu.

“Mwaka huu tunatarajia kuzalisha vizuri kufuatia ukweli kuwa mbolea tunayo ya kutosha” Kauku alisema

“Uwepo wa mbolea ya ruzuku kutatuwezesha kuhudumia shamba vizuri na kuzalisha kahawa bora kutakakopelekea kuzalisha kahawa nzuri” Kauku aliongeza.

Akielezea upande wa mavuno, Kauku anasema mavuno kwa shamba zima ni tani 150 – 180 kwa msimu uliopita wa kilimo na kubainisha kuwa kwa mwaka huu wanatarajia kuvuna tani 200 hadi 250.

” Mbolea ya ruzuku inasaidia sana si kwa kahawa tu na hata kwa mazao mengine na hivyo kupunguza bei ya nafaka kufuatia wingi wa mazao”Kauku ameendelea kusisitiza manufaa ya mbolea ya ruzuku kwa wakulima.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Karia  Magaro anasema mchango wa mazao kwenye mapato ya wilaya ni bilioni 2.4 na kueleza uwepo wa ruzuku ya mbolea utapelekea kuongezeka kwa mapato yatokanayo na kilimo kwani wakulima wameongeza maeneo ya kilimo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here