Na MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA, DODOMA
BAADA ya Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumaliza uhai wake wa kipindi cha miaka miwili na nusu, Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson, amewapanga upya wabunge hao katika kamati mbalimbali.
Hatua hiyo ni kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge, ambapo baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, wabunge hao usiku huu walikutana katika kumbi mbalimbali za Bunge kuchagua wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati hizo.
Miongoni mwa waliochaguliwa kuongoza kamati za kudumu za Bunge ni Pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, ambaye amechaguliwa akiwa mgombea pekee kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Michezo na Utamaduni na makamu wake akiwa ni Mbunge wa Viti Maalumu, Husna Sekiboko.
Wengine waliochaguliwa kuongoza kamati hizo ni pamoja na Mwenyekiti wa Bunge, David Mwakiposa Kihenzile ambaye amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo huku makamu wake akiwa ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Ditopile.
Kwa upande wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, alichaguliwa kuiongoza ni Mbunge wa Madaba, Joseph Mhagama na makamu wake Florent Kyombo huku Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alichaguliwa kuingoza ni Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa, makamu wake Vicent Mbogo.
“Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwenyekiti Denis Londo na makamu wake Lazaro Nyamoga. Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii itaongozwa na Fatma Hassan Toufiq na makamu wake Riziki Said Lulida.
“Kamati ya Maji na Mazingira Mwenyekiti Jackson Kiswaga huku makamu wake Anna Lupembe. Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii mwenyekiti ni Mbunge wa Korongwe Vijijini, Timotheo Mzava na makamu wake Ally Makoa wakati Kamati ya Afya na Masuala ya Ukimwi ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mbunge wa Maswa Mashariki, Stanlaus Nyongo makamu wake akiwa Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile.
Hata hivyo taarifa hiyo ya Bunge ilieleza kuwa kwa upande wa Kamati ya Miundombinu itaongozwa na Moshi Kakoso na makamu wake Anne Kilango huku Kamati ya Nishati na Madini ikiendelea kuongozwa na Mbunge wa Mkinga, Dastan Kitandula na makumu wake Judith Kapinga.
Kwa upande wa Kamati ya Bajeti itaongozwa na Daniel Sillo na makamu wake Mbunge wa Kilindi, Omari Kigua na kamati ya Sheria Ndogo itaongozwa na Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rwekiza makamu wake Ramdhan Ramadhan.
Naye Mbunge wa Ukonga, Jerry Sillaa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Uwekezaji na Mitaji ya Umma na makamu wake Augustino Vuma, mbali na hilo pia Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) itaongoza na Mbunge wa Viti Maalumu, Naghenjwa Kaboyoka (Chadema), makamu Japhet Hasunga, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ikiongoza na Halima Mdee na makamu wake Mbunge wa Nyamagana, Stanlaus Mabula na kwa upande wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itaongozwa na Ali Juma Makoa huku makamu wake Dk. Thea Ntara