Home KIMATAIFA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AONGOZA KAMATI YA UANGALIZI YA SADC NCHINI LESOTHO

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AONGOZA KAMATI YA UANGALIZI YA SADC NCHINI LESOTHO

Google search engine
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakata Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akiwa na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Makamu wa Rais Mstaafu wa Mauritius Paramasivum Pillay Vyapoory Pamoja na Ujumbe wa Seneti ya Lesoth alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo kuanzia Februari 8 hadi 11, 2023

Na MMWANDISHI MAALUMU

RAIS Mstaafu wa Awamu wa Nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panelof Elders, POE) ameongoza Ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatilia Utekelezaji wa Makubaliano ya Amani nchini Lesotho katika ziara nchini humo Februari 8 hadi 11 ,2023.

Ziara ya Kamati hiyo ya Uangalizi ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika Mkutano wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika Kinshasha nchini Jamhuri ya Kimokrasia ya Kongo (DRC) Agosti mwaka 2022 ambapo walilielekeza baraza hilo la Wazee la SADC kufuatilia kwa karibu jitihada za usuluhishi wa migogoro inayoendelea kwa muda mrefu katika Falme za Lesotho na Eswatini.

Rais Mstaafu Kikwete ameongozana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Mauritius, Paramasivum Vyapoory, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wazee amepata wasaa wa kukutana na Mtukufu Motlotlehi Letsie III, Mfalme wa Lesotho, viongozi wakuu wa Serikali ya Lesotho pamoja na wadau wengine muhimu katika mgogoro huo.

Kamati pia imepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Lesotho ambaye ndiye Mkuu wa Serikali, Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Haki, Sheria na Masuala ya Bunge, Spika wa Bunge, Makamu Rais wa Seneti, Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko, Viongozi wa Vyama vya Siasa vya Upinzani vilivyo Bungeni, Vyama vya Siasa vilivyo nje ya Bunge, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Askofu Mkuu wa Baraza la Kanisa la

Kikristu nchini Lesotho pamoja na Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Marekani, Uingereza, AfrikaKusini na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa.

Katika mikutano yote iliyofanyika, Kamati hiyo imesikiliza kwa kina maoni ya wadau hao wote kuhusu namna bora zaidi ya kuweza kuendeleza kazi nzuri ambayo tayari imeshafanyika katika kupata suluhu ya kudumu ya mgogoro uliopo nchini humo. Kamati hiyo inaripoti kwa Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika) ambaye kwa sasa ni Hage Geingob,Rais wa Namibia.

Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakata Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders) akikutana na Mabalozi wa Uingereza na wa Umoja wa Ulaya alipoongoza ujumbe wa Kamati ya Uangalizi ya SADC inayofuatia makubaliano ya amani nchini humo.
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here