Home MICHEZO TANZANIA MIPANGO UJENZI WA ‘SPORTS ARENA’ DAR

TANZANIA MIPANGO UJENZI WA ‘SPORTS ARENA’ DAR

Google search engine
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa Akizungumza na Wanahabari leo Februari 14,2023 mara baada ya kukabidhiwa eneo la hekari 12 litakazotumika kujenga Ukumbi wa Kimataifa wa Michezo (Sports Arena) Tanganyika packers Kawe Jijini Dar es salaam akisisitiza kuwa Mkandarasi ataanza ujenzi mapema Machi, 2023.

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mohamed Mchengerwa amesema Watanzania wana kiu ya kuona ukumbi wa Kimataifa wa Michezo ( Sports Arena) inajengwa nchini huku akieleza kwamba tayari Wizara imepokea hekari 12 eneo la Kawe jijini Dar es salaam kwa ajili ya ukumbi huo.

Akizungumza leo  Februari 14, 2023, Waziri Mohamed Mchengerwa wakati akikabidhiwa hekari hizo 12 , amesema kuwa Sports Arena itakayojengwa Kawe utakuwa na uwezo wa  kubeba watu 16000 na hivyo kutoa nafasi pia ya Watanzania kushuhudia matamasha mbalimbali yatakayokuwa yakifanyika katika ukumbi huo.

Aidha, Waziri Mchengerwa ameeleza kwamba  dhamira ya Dk. Samia Suluhu ni kuhakikisha sekta ya burudani na michezo zinakuwa sekta zinazokwenda kuchangia pato la Taifa.

“Watanzania wamekuwa wakihoji kuwa tayari Bajeti imepitishwa lakini hawaoni utekelezaji wa ujenzi wa ukumbi huo, lakini tuwatoe hofu kuwa sasa tunaenda kuandika historia nchini Tanzania kujengwa kwa ukumbi huo wa Kimataifa,” amesema Waziri Mchengerwa.

Pia ameeleza Arena hiyo inatarajiwa kukamilika kati ya Agosti na Oktoba mwaka huu na utakuwa moja ya ukumbi mkubwa barani Afrika kama ilivyo Arena kubwa ya nchini Senegal inayochukua watu 15000.

“Tulipotoka hatukuwa na mipango mizuri hivyo tulivyoingia na Wasaidizi  wetu tumehakikisha tunaenda kuongeza nguvu kubwa tutengeneze mipango yetu, tutengeneze michoro na hatua zote tumekwisha kuzikamilisha na tunatarajia mwezi Machi mwaka huu kumkabidhi Mkandarasi na ujenzi.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba Wizara itahakikisha inasimama kidete  hadi kukamilisha maagizo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kukamilisha ujenzi huo wa ukumbi wa Arena nchini Tanzania.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa Akizungumza na Wanahabari leo Februari 14,2023 mara baada ya kukabidhiwa eneo la hekari 12 litakazotumika kujenga Ukumbi wa Kimataifa wa Michezo (Sports Arena) Tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es salaam akisisitiza kuwa Mkandarasi ataanza ujenzi mapema Machi, 2023
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here