“Tumejipanga na tunakuja na mkakati kabambe kumaliza Migogoro ya wakulima na wafugaji, nataka tuandike pamoja historia ya kumaliza kabisa changamoto ya migogoro hii Kilosa. Na mimi nikiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hii nitaanza na watendaji ndani ya serikali ambao ni sehemu ya ustawi au wanufaika wa migogoro hiyo, hivyo niwahahakishie kama kuna mtu yeyote miongoni mwetu, anafaidika na migogoro hii ama anahusika kwa namna moja ama nyingine kuistawisha atakutana na mkono mkali wa sheria kwenye hili hatutangaliana usoni,” DC Shaka Hamdu Shaka