Home KITAIFA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUKWEPA KODI

WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUKWEPA KODI

Google search engine

NA MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

WATU wawili, Sibtain Murji 43 na Zameen Murji 47 wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikalibiwa na mashtaka matatu likiwemo la kukwepa kodi kiasi cha Sh. Bilioni sita.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Sylivia Mitanto akisaidiana na wakili Emmanuel Medalakini imedai kuwa tarehe isiyojulikana kati ya Januari 2021 Desemba 2022 jijini Dar es Salaam washtakiwa walishundwa kupeleka tamko la Mapato la biashara iliyosajiliwa kwa jina la Murji Brothers na kupelekea kukwepa kodi ya Sh bilioni 6.2

Pia inadaiwa, siku na mahali hapo washtakiwa hao kwa pamoja kwa makusudi, walikwepa kodi kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia Mamlaka ya Mapato (TRA) hasara ya kiasi cha fedha zaidi ya Sh bilioni 6.2

Katika shtaka la utakatishaji fedha inadaiwa, Sikh na mahali hapo washtakiwa hao walijipatia kiasi hicho cha fedha cha sh. bln 6/- huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kukwepa kodi.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 3, 2023.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here