Home KITAIFA AFDB YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME NCHINI

AFDB YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME NCHINI

Google search engine
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Umeme Wizara ya Nishati, Mhandisi Christopher Bitesigirwe (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayewakilisha nchi ya Tanzania, Ronald Cafrine, (wa tatu kushoto), wakati wa ziara ya kukagua miradi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Zuzu, mkoani Dodoma.
Mhandisi Mkuu wa Umeme katika Mradi wa kusafirisha umeme wa Msongo Mkubwa, Adolph Kigombola(kulia) akimuonyesha Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayewakilisha nchi ya Tanzania, Ronald Cafrine,(wa pili kulia),namna umeme unavyoingia katika Kituo cha Kupoza na Kupokea umeme cha Zuzu wakati wa ziara ya kukagua kituo hicho, Februari 23,2023 mkoani Dodoma . Kushoto ni Mhandisi Edson Ngabo kutoka Wizara ya Nishati anayesimamia miradi ya Malagarasi Kakono na mradi wa Nyakanazi- Kigoma inayofadhiliwa na Benki ya AfDB.

Na Zuena Msuya, Dodoma

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayewakilisha nchi ya Tanzania, Ronald Cafrine amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini hususani miradi ya Nishati.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha Kupokea na Kupoza umeme cha Zuzu mkoani Dodoma ambao Benki hiyo imeshiriki kuchangia ufadhili wa gharama zilizotumika katika ujenzi wa kituo hicho iliyofanyika Februari 23, 2023.

Katika ziara hiyo, Cafrine aliambatana na ujumbe wake pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Cafrine alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi ya umeme inayofadhiliwa na Benki hiyo ili kujionea utekelezaji wake na hatua iliyofikiwa kutokana na fedha zinazotolewa na Benki hiyo.

Baada ya kuona hali halisi ya utekelezaji wa miradi hiyo, ameeleza kuwa miradi hiyo imefikia hatua nzuri za utekelezaji wake, pia AfDB imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ya Ujenzi, Maji na Nishati.

Ameipongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake kwa usimamizi mzuri wa fedha zinazotolewa na Benki hiyo katika kutekeleza miradi husika.

Ameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Sita katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Kaimu Kamishna Msaidizi wa umeme, Mhandisi Christopher Bitesigirwe amesema Tanzania kama nchi inayoendelea kukua inahitaji zaidi nishati ya umeme katika kuhakikisha kuwa uchumi wake unakua na kufikiwa kiwango kitachotakiwa duniani, kwa kuwa na umeme wa uhakika, wakutosha na wa gharama nafuu ili kutimiza malengo iliyojiwekea.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa AfDB, imetoa mchango mkubwa katika miradi ya kuzalisha, kusambaza na kusafirisha umeme katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo miradi ya kufua umeme kwa kutumia maji ya Kakonko, Malagarasi, mradi wa kusafirisha umeme mkubwa wa msongo wa Kilovolti 400 kutoka Iringa – Dodoma – Shinyanga hadi Namanga, mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 220 kutoka Rusumo hadi Nyakanazi, na mradi wa msongo wa Kilovolti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayewakilisha nchi ya Tanzania, Ronald Cafrine, (kushoto), akiteta jambo na Mhandisi Salma Bakari wa Wizara ya Nishati (wa pili kushoto), wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa Kituo cha Kupokea na Kupoza umeme cha Zuzu
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here