MGOMBEA wa chama tawala nchini Nigeria Bola Tinubu anaongoza katika uchaguzi wa urais baada ya matokeo kutolewa katika majimbo 14 kati ya 36 ya nchi hiyo.
Bw Tinubu ameshinda zaidi ya 44% tu ya kura zilizohesabiwa.
Wakati mpinzani wake mkuu Atiku Abubakar ana karibu 33% ya kura.
Peter Obi wa chama cha Labour ana karibu ya 18%, baada ya kusababisha hasira kwa kumshinda Bw Tinubu katika jiji kubwa zaidi la Lagos.
Jumatatu, Chama cha Bw Abubakar na chama cha Bw Obi vilitoka nje ya ukumbi wakati matokeo yanatangazwa.
Chama cha Peoples Democratic Party (PDP) na chama cha Labour vimedai kuwa kuna ukosefu wa uwazi na mfumo mpya wa kielektroniki wa wapiga kura.
Huu ulikuwa uchaguzi wa kwanza wa kitaifa ambapo kifaa cha kielektroniki kilikuwa kimetumika kuwaidhinisha wapiga kura.
Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (Inic) imekanusha malalamiko ya vyama hivyo vya upinzani.
Mwenyekiti wake Mahmood Yakubu alisema utangazaji wa matokeo utaendelea.
Waangalizi wa Umoja wa Ulaya walisema mipango na mawasiliano duni ya shirika la uchaguzi inadhoofisha imani katika mchakato huo.