Vikosi vya Urusi siku ya Jumanne vimeendelea na safari yao ya wiki moja ya kuuzingira na kuuteka mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine ambapo kamanda wa vikosi vya ardhi vya Ukraine alielezea hali kuwa “ya wasiwasi mkubwa”.
Wanajeshi wa Urusi, wakiwemo wapiganaji kutoka Kundi la Wagner, wanajaribu kuzuia njia za watetezi wa Ukraine katika mji huo, eneo la vita lenye umwagaji damu mkubwa zaidi katika vita hivyo, na kuwalazimisha kujisalimisha au kujiondoa.
Hilo litaipa Urusi tuzo yake kuu ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya nusu mwaka na kufungua njia ya kudhibiti miji ya mwisho ilivyobaki katika eneo la Donetsk, moja kati ya minne ambavyo Moscow inadai kuichukua katika kile inachokiita “operesheni yake maalum ya kijeshi, ” nchini Ukraine.
“Licha ya hasara kubwa, maadui walirusha mashambulizi yaliyoandaliwa zaidi na Wagner, ambayo yanajaribu kuvunja ulinzi wa wanajeshi wetu na kuuzingira mji,” Kanali Mkuu wa Ukraine Oleksandr Syrskyi alisema katika taarifa.
Mwanajeshi ambaye jina lake halikutajwa kutoka Kikosi cha 93 cha Mechanised Brigade cha Ukraine, akiongea kwenye programu ya ujumbe wa Telegram huku milipuko ikitokea nyuma, na kusema “Februari 28, mji wa Bakhmut.
Jiji linawaka moto, adui anasonga mbele. Kila kitu kitakuwa Ukraine…” Shirika la habari la serikali ya Urusi la RIA lilitoa kipande cha video ambacho kilisema kilionyesha ndege za kivita za Urusi aina ya Su-25 zikiunguruma juu huko Bakhmut.
“Tunafurahi kuwa ni zetu,” anasema mwanamume mmoja kwenye kipande hicho cha video aliyetambuliwa kama mpiganaji wa Wagner, akiongeza ndege hizo ziliwasaidia “kisaikolojia.”
Jeshi la Ukraine lilisema Urusi ilikuwa inashambulia makazi karibu na Bakhmut, ambayo ilikuwa na wakazi wapatao 70,000 kabla ya vita lakini sasa ni magofu baada ya miezi kadhaa ya vita vikali.
“Katika siku iliyopita, askari wetu walizuia zaidi ya mashambulizi 60 ya adui,” jeshi lilisema mapema Jumanne, ikiwa ni pamoja na katika vijiji vya Yadhidne na Berkhivka kaskazini mwa Bakhmut.
Mwandishi wa Reuters ambaye alitembelea eneo hilo siku ya Jumatatu alisema haoni dalili zozote za vikosi vya Ukraine kuondoka na kwamba vikosi vya ulinzi vilikuwa vikiwasili licha ya mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi.