Home KITAIFA Kikwete ana kwa ana na Tume ya Haki Jinai

Kikwete ana kwa ana na Tume ya Haki Jinai

Google search engine

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete amewasili katika Ukumbi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) leo Ijumaa Machi 31, 2023 tayari kwa mahojiano na Tume ya kuangalia mfumo wa haki jinai.

Kikwete amewasili ukumbini hapo saa 4:23 asubuhi na kupokewa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Mohammed Chande Othman na Wajumbe wengine.

Kwa mujibu wa Tume hiyo, Rais huyo mstaafu ndiye mjumbe wa mwisho kupokea maoni yake baada ya makundi mbalimbali kusikilizwa.

Baada ya kuwasili alifikishwa katika moja ya chumba kabla ya dakika tano baadaye kupelekwa katika ukumbi maalum wa kutoa maoni hayo.

Tume hiyo iliyoanza kazi Februari 6,2023 imeshafanya mahojiano na makundi mbalimbali katika Mikoa 14 na Wilaya 30.

Baada ya Kikwete, kinachosubiriwa kwa hamu ni ripoti ya Tume hiyo iliyopangiwa kufanya kazi kwa siku 120.

Kabla ya Kikwete wengine viongozi wengine mbalimbali walishatoa maoni yao, akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here