Uamuzi wa Rais wa Kenya William Ruto wa kubadili msimamo wake mkali wakati kukiwa na maandamano ya upinzani ulifungua milango ya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameambia BBC.
Siku ya Jumapili Rais Ruto alihutubia taifa kwa mara ya kwanza tangu maandamano yaanze kuhusu gharama ya juu ya maisha na madai ya ukiukaji wa taratibu za uchaguzi.
Rais alikubali mojawapo ya matakwa ya Bw Odinga- ushirikiano wa pande mbili bungeni kuhusu kubuniwa kwa tume ijayo ya uchaguzi.
Lakini alipendekeza hatamshirikisha kiongozi wa upinzani katika matakwa yake mengine, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama ya maisha na uhalali wa urais wake.
Katika mahojiano na BBC, Bw Odinga alimkaribisha “kujishusha” na kumsisitiza Bw Ruto kwamba masuala yote lazima yawekwe mezani.
Soma zaidi: