Home KIMATAIFA Umoja wa Mataifa ‘una wasiwasi mkubwa’ kuhusu mpango wa hifadhi ya Rwanda

Umoja wa Mataifa ‘una wasiwasi mkubwa’ kuhusu mpango wa hifadhi ya Rwanda

Google search engine

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema bado “ina wasiwasi mkubwa kuhusu athari” ya serikali ya Uingereza kutuma baadhi ya wahamiaji nchini Rwanda iwapo watawasili Uingereza kupitia njia zisizo halali.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman amesisitiza kuwa Rwanda ni nchi salama kwa wahamiaji.

Alisema siku ya Jumapili kwamba anaamini sera ya Rwanda itakuwa na “athari kubwa ya kuzuia” ili watu waache kusafiri kwa njia za mashua hadi Uingereza.

Lakini ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema tathmini zilizofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi zilionyesha kuwa mfumo wa hifadhi nchini Rwanda “sio imara vya kutosha”.

“Pia kuna wasiwasi kuhusu kuheshimiwa kwa uhuru wa kukusanyika na uhuru wa kujieleza nchini Rwanda. Wasiwasi huo bado upo leo,” msemaji Ravina Shamdasani aliambia kipindi cha Newsday cha BBC.

“Tuna ushahidi mwingi wa jinsi mipango hii [mifumo ya hifadhi ya nje ya pwani] inaharibika,” aliongeza.

Unaweza pia kusoma

Kutupeleka Rwanda haukutuzuia kufika Ulaya

Tazama: Rwanda inavyowawezesha wakimbizi kubuni nafasi za kazi

Uhamiaji: Kwanini Uingereza inawapeleka waomba hifadhi Rwanda?

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here