Home KITAIFA Waliogushi vyeti walamba Sh bilioni 35.02 malipo zaidi yakiendelea

Waliogushi vyeti walamba Sh bilioni 35.02 malipo zaidi yakiendelea

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

WAKATI wimbo la walioghushi vyeti likiendelea kipasua kichwa Serikali, imebainika jumla ya Sh bilioni 35.02 zimelipwa kwa watu 11,896 waliokuwa wafanyakazi ambao waliondolewa kwa kosa la kughushi vyeti.

Imeelezwa kuwa fedha hizo zimelipwa kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PSSSF baada ya agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kwamba wahusika walipwe.

Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwasilisha Hotuba ya Maombi ya Makadilio ya Mapato na matumizi ya 2023/24 kwa wizara na taasisi zilizochini yake.

Fedha hizo ni sehemu ya michango ya waliokuwa wafanyakazi hao ambao walioondolewa kwa kukosa sifa lakini akasema Serikali inaendelea kulipa kwa kadri inavyopata taarifa kutoka kwa wahusika.

Kutokana na hali hiyo Majaliwa amesema hadi Februari mwaka huu, jumla ya Sh trilioni 2.17 zilikuwa zimelipwa kwa PSSSF ambalo lilikuwa ni deni.

Kuhusu malipo ya wastaafu, Waziri Mkuu amesema Shtrilioni 1.74 zililipwa kwa Wastaafu 41,949 wa mfuko wa PSSSF ambapo wastani wa malipo kwa mwezi ni Sh bilioni 63.4.

Katika hotuba yake hiyo ya bajeti amesema kwa upande wa NSSF alitaja wastaafu 43,832 waliolipwa Sh72 bilioni kwa kipindi hiki sawa na wastani wa Sh bilioni 9.04 kwa kila mwezi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here