Home KITAIFA Dk. Tulia ataitaka Serikali kutoa ajira kwa wanaojitolea

Dk. Tulia ataitaka Serikali kutoa ajira kwa wanaojitolea

Google search engine
Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

Spika wa Bunge la Dk.Tulia Ackson, ameitaka Serikali kupitia Wizara za Afya, TAMISEMI pamoja na Ofisi ya Rais Utumishi kuangalia upya utaratibu wa utoaji wa ajira kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele kwa watu wanaojitolea kufanya kazi bila malipo katika nafasi hizo.

Dk. Tulia ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma, wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa kumi na moja wa Bunge unaoendelea.

“Huwa haipendezi sana zinapotangazwa ajira mpya zinapotolewa unakuta wale watumishi wote waliokuwa wakijitolea katika nafasi hizo hakuna hata mmoja aliyepata. Sasa huwa tunajiuliza ni kwamba wale wanaojitolea hawana sifa na waliopo nyumbani ndio wanasifa zaidi,” amesisitiza Dk.Tulia

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here