Home KITAIFA Dk. Jafo: Matumizi ya mkaa mwisho Januari 2024

Dk. Jafo: Matumizi ya mkaa mwisho Januari 2024

Google search engine

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

SERIKALI imetangaza kuwa ifikapo Januari 31,2025 utakuwa mwisho matumizi ya kuni na mkaa ili kulinda mazingira na ukataji miti nchini.

Agizo hilo limetolewa leo Jumatano, Aprili 12 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Seleman Jafo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kulinda mazingira

Dk Jafo amesema taasisi zote ambazo zinahudumia watu wasiopungua 100, mwisho wao wa kutumia kuni na mkaa utakuwa ni Januari 31, 2024 na wanaohudumia watu kuanzia 200 mwisho wao ni Januari 31,2025.

Waziri Jafo amesema zaidi ya Hekta 46,960 ambayo ni asilimia 26 ya ardhi huharibiwa kila mwaka kutokana na ukataji wa miti kwa matumizi ya kuni na mkaa jambo ambalo ni hatari kwa kuwa linamaliza misitu.

“Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, inakadiriwa kuwa asilimia 16 ya ardhi imeharibika na inakabiliwa na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kutokana na watu wengi kufanya shughuli zisizoendelevu ikiwemo kutumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia,” amesema Jafo.

Amesema nishati ya kuni hutumika kwa wingi kwa sababu ni rahisi kupatikana na watu wengi wanaweza kumudu gharama yake tofauti na nishati nyinginezo kama vile umeme na gesi.

Hata hivyo amesema licha ya unafuu wake lakini upatikanaji wa nishati hiyo na matumizi yake yanaathiri afya ya mtumiaji kwa kusababisha magonjwa yatokanayo na kuvuta hewa chafu inayoathiri mapafu, moyo na magonjwa ya kupumua kwa watoto.

Amesema Serikali imeweka mkakati wa kupunguza athari hizo kwa kuandaa Dira ya Taifa ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Dira hiyo kwa kipindi cha miaka kumi hadi kufikia 2033.

“Kwa Mamlaka niliyopewa chini ya Kifungu cha 13 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura ya 191, natoa Katazo Kwa Taasisi zote za Umma,na Binafsi Tanzania Bara zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi ya 100 kwa siku kusitisha matumizi ya kuni na mkaa ifikapo Januari 31,Januari, 2024, Aidha, Taasisi zinazoandaa Chakula na kulisha watu zaidi ya 300 kwa siku kusitisha matumizi ya kuni na mkaa ifikapo Januari 31, 2025,” amesema Jafo.

Waziri amezitaka kampuni za gesi, mkaa mbadala na majiko banifu kutumia katazo hilo kama fursa ya uzalishaji ili kuwasaidia wahitaji.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here