Home KITAIFA Gavana Tutuba awataka Watanzania kuchapa kazi

Gavana Tutuba awataka Watanzania kuchapa kazi

Google search engine
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, akizungumza wakati wa Iftari iliyoanfaliwa na BoT jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amewahimiza Watanzania kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji na hivyo kukuza uchumi.

Hayo ameyasema leo katika hafla ya futari aliyowaandalia viongozi wa Serikali, Jumuiya ya wenye Mabenki, Watoto wa Madrasa na Makundi Maalum kwenye Makao Makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam Aprili 20, 2023.

“Sisi kama Benki Kuu tunaendelea kusimamia uchumi wa nchi  yetu  na niwahakikishie uchumi wetu uko imara, mfumuko wa bei umedhibitiwa na fedha yetu pia iko imara, sekta ya fedha inazidi kukua.

“… “Ninachoomba kutoka kwenu ni ushirikiano, tufanye kazi kwa bidii ili tuzalishe zaidi kwani hiyo ni nyenzo muhimu katika kujenga uchumi imara.” amesema

Gavana huyo wa BoT alisema Benki Kuu ya Tanzania kwa umakini mkubwa itaendelea kusimamia ustahimilivu  wa uchumi, sera ya fedha, mfumuko wa bei,utoaji wa leseni kwenye taasisi za fedha, udhibiti sekta ya fedha na usimamizi wa mauzo ya nje.

“Juzi nilikuwa kwenye Mikutano ya Benki ya Dunia (WB) wameisifu nchi yetu kwa usimamizi mzuri wa uchumi ikilinganishwa na Mataifa mengine.” Alidokeza.

Aidha Gavana Tutuba aliwashukuru wote walioitikia mwaliko wa BoT kuja kujumuika na watumishi wa Benki hiyo katika sadaka hiyo ya futari.

Tukio kama hili tunalifanya kwenye matawi yetu yote Saba (7) na lengo kwakweli ni kuungana na jamii katika kufanya matendo mema yanayompendeza Mungu.

“Kufunga, kusali  kutoa sadaka ni mambo ambayo Mwenyezimungu huyapokea kwa haraka.” amesema Tutuba.

Awali akitoa Mawaidha kuhusu “Uislamu na Uchumi” kabla ya futari, Imam wa Msikiti wa Maamour Upanga jijini Dar es Salaam, Sheikh Issa Othman (Mufti London), alisema ipo misingi sita (6) inayoelezea Uislamu na Uchumi ambayo ni udugu, Naswiha, kuheshumu makubaliano, Hofu ya Mungu, na huruma.

Sheikh Othman pia amesema, Nidhamu ni jambo muhimu sana katika Uislamu.

 Funga ya Mwezi Mtukufu wa Radhan, inajenga nidhamu binafsi mambo ambayo yanahimizwa katika uislamu.

Akifafanua amesema, Nidhamu hiyo imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni active diceplin, reactive dicepli (inafundisha ustahikilivu kwamba hata unapochokozwa hupaswi kujibiza na mwisho ni proactive deciplin (mambo ambayo umeyazingatia au kuyafuata wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uendelee kuyafuata hata baada ya kumalizika kwa Mfungo.

Naye Sheikh Muharram Mziwanda aliwahimiza Watanzania kwa ujumla kuendelea kuenzi Amani na Utulivu nchini kwani mafanikio ya kukua kwa uchumi yanategemea sana hali ya Amani na Utulivu wa nchi.

 “Uchumi hauwezi kusogea ikiwa Msingi wa uchumi haupo (utulivu), tuhakikishe tunaendelea kuenzi Amani na Utulivu kila mmoja kwenye nafasi zetu,” amesema Sheikh Mziwanda.

Imam wa Msikiti wa Maamour Upanga jijini Dar es Salaam, Sheikh Issa Othman (Mufti London)
Waalikwa wakiwa kwenye Iftar iliyoandaliwa na BoT jiji ni Dar es Salaam
Sehemu ya waalikwa na wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wakiwa kwenye Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo jijini Dar es Salaam
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here