Home KITAIFA Sababu hizi zamfanya Dk. Tulia kuomba kugawanywa jimbo

Sababu hizi zamfanya Dk. Tulia kuomba kugawanywa jimbo

Google search engine
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson

Na Mwandishi Wetu

-Dodoma

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawanywa kwa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.

Hilo limeibuka leo Mei 3, 2023 Bungeni Jijini Dodoma katika taarifa iliyolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda.

Katika swali lake Mwakagenda ameuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.

“Kama Serikali tunatambua lakini nikuhakikishie, Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye ni Spika wetu Tulia ameshawasilisha suala hili na lipo mezani kwahiyo muda utakapofika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatizama pia Jimbo la Mbeya Mjini.” Amesema Naibu Waziri Ummy akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda.

Katika swali la msingi mbunge wa Kilindi Omari Kigua ameuliza ni lini Serikali italigawa Jimbo la Kilindi kutokana na jiografia yake.

Naibu Waziri amesema kwa sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi mbalimbali  ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

“Hivyo kwa kuzingatia taratibu na vigezo, muda wa kugawa majimbo utakapofika Tume itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa machakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao na hivyo kushughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kikatiba,”amesema Ummy.

Naibu Waziri Ummy,  amesema majimbo mengi yameomba kugawanywa lakini mambo yanayotazamwa ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa Bunge, idadi ya wabunge wa viti maalumu na jiongrafia za maeneo yaliyoomba kugawanywa.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here