Home KITAIFA Makamba afanya mazungumzo na kampuni zitakazotekeleza mradi wa LNG

Makamba afanya mazungumzo na kampuni zitakazotekeleza mradi wa LNG

Google search engine
Waziri wa Nishati, January Makamba ( wa Tano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Medco Duniani,  Roberto Lorato  ( kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Pavilion Energy ltd, Alan Heng wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusindika Gesi Asilia (LNG) kilichofanyika mkoani Dodoma , Aprili 9,2023.
Waziri wa Nishati, January Makamba (kushoto) akiongoza kikao kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusindika Gesi Asilia( LNG), kilichowashirikisha Wawekezaji watakaotekeleza Mradi huo waliopo upande wa kulia ambao Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Medco Energi, Roberto Lorato, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Pavilion Energy ltd, Alan Heng, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Shell nchini Tanzania, Jared Kuel, upande wa kushoto kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Athumani Mbuttuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Mussa Makame na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Nishati, kilichofanyika mkoani Dodoma , Aprili 9,2023.

Na Zuena Msuya, Dodoma

Waziri wa Nishati, January Makamba amekutana na Viongozi wa Kampuni zitakazotekeleza Mradi wa kuchakata na kusindika Gesi ya Asilia (LNG).

Makamba amekutana na viongozi hao ambao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Medco Energi, Roberto Lorato, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Pavilion Energy ltd, Alan Heng pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Shell nchini Tanzania, Jared Kuel kwa lengo la kujadili maendeleo ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa LNG.

Mkutano huo umefanyika Aprili 9, mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Athumani Mbuttuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania Mussa Makame na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Nishati.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Medco Energi, Roberto Lorato amesema kampuni hizo ziko tayari kuanza utekelezaji wa mradi huo mara baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Kwa upande wake, Waziri Makamba amezihakikishia kampuni hizo kuwa Serikali iko tayari kuutekeleza mradi huo Mkubwa na wa kimkakati kwa manufaa makubwa nchini.

Alifafanua kuwa mradi huo utakaogharimu zaidi ya shilingi Trilioni 70 za kitanzania ni muhimu kwa taifa katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo zaidi.

Vilevile aliwahakikishia wawekezaji kuwa  Serikali imeanza maandalizi ya utekelezaji wa Mradi kwa kuanzisha Ofisi Maalum  (LNG Project Office)ili kurahishisha uratibu wa masuala yote ya Mradi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here