Na Mwandishi Wetu
-Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amehidi kukaa meza moja na Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) pamoja na wamiliki wa baa kama njia ya kutafuta mwafaka wa pamoja.
Hatua hiyo inakuja baada ya NEMC kuanza oparesheni tangu Mei Mosi mwaka huu kuzifungia baa ambazo zimekuwa zikipiga keleke kinyume cha sheria na vipimo vya uchafuzi wa mazingira kwa kelele.
Akizungumza leo Mei 16, 2023 baada ya kutembelea maeno kadhaa ya wafanyabishara jijini hapa, amesema kuwa ataendelea kushirikiana na NEMC ili kujadiliana na hali ya kuzifungia baa kwani kwa sasa ukaguzi wa baa hasa zinzokiuka kesheria kupiga muziki kinyume cha sheria ikipamba moto
“Ninashukuru kwamba Dar es Salaam ndio kitovu cha starehe kila jambo lina utaratibu wake, kitu ambacho nimekiona nimeona NEMC akiendesha oparesheni jambo itanipasa kukaa nao pamoja ili kuweza kujadiliana kwa kina lengo si kuvunja sheria.
“kikubwa ninachoangalia bia ni uchumi, kwenye bia ni ajira kwani kuna viwanda vingapi vinazaliasha ajira, ila starehe isigeuze karaha. Tutakaa mimi na NEMC pamoja na wasaidizi wangu kwani ninaamini kuna watu wamekopa fedha ili angalau kuendesha baa,” amesema