Na Mwandishi Wetu
-Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana amesema mgomo unaoendelea leo unasababishwa na kikundi cha watu wachache wenye maslahi yao binafsi.
Kutokana na hilo amesema kama kiongozi yuko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili viweze kuwachukulia hatua watu hao.
Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 15, 2023 wakati akizungumkutokana na baadhi ya maduka kuendelea kufungwa, licha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana kuwataka wafanyabiashara hao kusitisha mgomo huku akiahidi kushughulikia kero zao kikao cha kesho Jumatano ya Mei 17, 2023.
Kauli ya Mwenyekiti huyo inakuja ikiwa baadhi ya maduka katika soko hilo bado kufungwa kwa siku ya pili sasa.
Katika hilo imebaiika kuwa maduka yaliyofungwa, ni yale yanayouza nguo, viatu, vyombo, vitenge, mapazia huku yaliyofunguliwa yakiwa ni yale ya vifaa vya magari, urembo wa ndani, na maduka ya vitambaa vya kushona.
Hata hivyo maduka mengi yaliyowazi, ni yale yaliyopo pembezoni mwa soko huku asilimia kubwa ya maduka ya katikati yakiwa yamefungwa.
Amesema kilio chao kama wafanyabiashara ilikuwa ni kusikilizwa na Rais Samia Suluhu Hassan, na katika kuonyesha kuwa amewasikia alimtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
“Alipokuja aliwaomba wafanyabiashara wafungue maduka na kuahidi kuwasiliza siku ya Jumatano. Nashangaa wafanyabiashara kuwa hawana imani na Waziru Mkuu,” amesema
Amesema shida ni kikundi cha watu wachache wanaoonekana kuwa na manufaa na mgomo huo huku akieleza kuwa ameomba msaada kwa vyombo vya usalama.
“Kuna kikundi cha watu wachache wanafaidika na huu mgomo ikiwemo kuonyesha kuwa kazi hazifanywi na Rais Samia Suluhu Hassan. Unafunga duka Rais ameshamtuna Waziri Mkuu, ametaka mfungue maduka bado hutaki; unataka nini!” Amehoji mwenyekiti huyo.
Miongoni mwa kero zilizokuwa zikilalamikiwa na wafanyabiashara hao, ni kamatakakamata ya wafanyabiashara, utoaji wa risiti xa kielektroniki na kudai kuwa unaua biashara. Wafanyabiashara hao pia wanalalamikia sheria mpya ya usajili wa stoo.
Mgomo huo ambao kwa mujibu wa viongozi wake, un lengo la kuishawishi serikali kusikiliza kilio chao, na hivyo serikali kuonyesha nia ya kukaa meza moja na wafanyabiashara hao, hali imekuwa tete kwa wafanyabiashara wanaonunua bidhaa sokoni hapo wakitoka nje ya Dar es Salaam.