Home KITAIFA TUZO ZA WATU NA MAZINGIRA (WaMa AWARDS) ZAZINDULIWA KWA KISHINDO

TUZO ZA WATU NA MAZINGIRA (WaMa AWARDS) ZAZINDULIWA KWA KISHINDO

Google search engine
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa TSDI, Fred Kwezi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Tuzo za Watu na Mazingira (WaMa Awards) leo Mei 22,2023 Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

-Dar es Salaam

TUZO za Watu na Mazingira (WaMa Awards) zimezinduliwa rasmi leo Mei 22,2023 Jijini Dar es Salaam ambapo tuzo hizo za kipekee zenye lengo kuu la kutambua na kuthamini juhudi za wadau mbalimbali katika Sekta ya Mazingira.

Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa TSDI, Bw.Fred Kwezi amesema tuzo hizo zimebuniwa na kuratibiwa na Asasi za Kiraia zikiwemo Tanzania Sustainable Development Initiative (TSDI), Human Dignity and Environmental Care Foundation (HUDEFO), Environmental Conservation Community of Tanzania (ECCT) pamoja na ELCA Environmental Consultancy.

Amesema tuzo hizo zinatoa fursa kubwa kwa makampuni, taasisi na wafanyabiashara binafsi kujitangaza na kukutana moja kwa moja na wadau mbalimbali katika sekta ya mazingira.

Amesema tuzo hizo zinatarajiwa kuwa ni tukio la kila mwaka kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo huadhimishwa Juni 5 (ya kila mwaka).

“Hafla ya kukabidhi tuzo itakuwa ni kilele kwani kabla itatanguliwa na matukio kadhaa yakiwemo Usafi katika fukwe na maeneo ya umma (wenye kulenga hasa kutoa elimu na ufumbuzi wa changamoto kadha wa kadha za kimazingira, Maonyesho ya bidhaa na huduma rafiki kwa mazingira (Eco-market showcase – exhibition), Mafunzo (darasani na field), Story telling – hamasa kutoka kwa watu waliofanikiwa, Kongamano (litalolenga kauli mbiu kwa mwaka husika) na usiku wa Tuzo ambayo ni kilele.

Aidha amesema jumapili na jumatatu Mei 28 & 29 kwa siku mbili mfululizo kutakuwa na maonyesho ya bidhaa na huduma rafiki kwa mazingira (Eco-market showcase – exhibition) katika viwanja vya posta eneo la sayansi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa HUDEFO Bi.Sarah Pima amesema wanatarajia kuona ushiriki kutoka nagzi tofautitofauti kwenye jamii, sekta binafsi, serikali na wadau ambao wapo kwenye asasi mbalimbali hivyo basi wanawakaribisha waweze kushiriki.
.
“Tumekuwa tukiona tuzo nyingine lakini kwenye upande wa mazingira mnyororo wake wa thamani tumekuwa tukiacha nyuma kwahiyo sasa tunapenda kuwatia moyo wadau wa mazingira na wananchi kwa ujumla waweze kushiriki na waweze kuziunga mkono tuzo hizi ili tuweze kuhifadhi na kutunza mazingira yetu vizuri”. Amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here