Home KITAIFA Hoja za Waitara zamng’oa RC Mara, Rais Samia amteua Said Mtanda

Hoja za Waitara zamng’oa RC Mara, Rais Samia amteua Said Mtanda

Google search engine
Rais Samia Suluhu Hassan

Na Mwandishi Wetu

-DAR E S SALAAM

SASA ni wazi kwamba hoja za Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, kuhusu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee zimefanikiwa kumng’oa katika nafasi hiyo

Kwa muda mrefu viongozi hao wamekuwa wakilumbana kuhusu suala la uwekaji wa alama kati ya hifadhi na vijiji vinavyotenganisha hifadhi ya Serengeti, jambo ambalo mara lilimfanya Meja Jenerali Mzee kumuonya Mbunge huyo na viongozi wa CCM kuhusu kupinga hatua hiyo ya Serikali.

Kutokana na hali hiyo ambayo ilizua sintofahamu Mbunge Waitara alipinga hatua hiyo hadharani huku akiungwa na mkono na wenyeviti wa vijiji ambao walitangaza kujiuzulu kutokana na kile walichodai ubabe wa Mkuu wa Mkoa

Mkuu wa Mkoa mteule wa Mara, Said Mtanda
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara

Kutokana na hali hiyo leo Mei 23, 2023 Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na kumteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Said Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akichukua nafasi ya Meja Jenerali Sulaiman Mzee ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Kauli hiyo ya Meja Jenerali Mzee, ilipingwa hadharani na mbunge Waitara pamoja na viongozi wa CCM Mkoa wa Mara na kuiona ni saw ana udhalilishaji wa chama na viongozi wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ilieleza kuwa  mbali na Rais Dk. Samia, pia amemuhamisha Queen Sendiga kwenda Mkoa wa Manyara akichukua nafasi ya Makongoro Nyerere ambaye naye amehamishiwa Mkoa wa Rukwa kuendelea na majukumu ya mkuu wa mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere

Pamoja na hili pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Kenani Kihongosi naye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo, akichukua nafasi ya Saidi Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Mkuu wa Wilaya Mteule, Kenani Kihongosi

Machi 29, mwaka huu ulitoa kauli na kuwaonya  viongozi wa kisiasa mkoani humo kuacha kuingilia kazi ya uwekaji vigingi kwenye mpaka baina ya vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika wilaya ya Tarime.

Onyo hilo lilitolewa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee wakati alipokuwa akizindua uwekaji wa vigingi hivyo, kazi inayotarajiwa kufanyika kwa muda wa siku 30.

Alisema inasikitisha kuona viongozi wa CCM, akiwamo Mbunge wa Tarime vijijini, Mwita Waitara kupinga kazi hiyo ambayo alisema inalenga kuleta suluhisho la kudumu kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya vijiji hivyo na hifadhi hiyo mgogoro uliodumu kwa zaidi miaka 40.

Kutokana na hali hiyo Mei 9, 2023 katika Bunge la Bajeti linaloendelea Mbunge wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara amelia bungeni akilalamikia kuwa Serikali wametoa majibu ya uongo kuhusu fidia ya Bunge ya wapiga kura wake waliotakiwa kupisha mgodi wa Barrick North Mara.

Hayo yalitokea baada ya Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato kujibu swali la msingi la mbunge huyo kwaniaba ya Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko.

Katika swali lake la msingi, Waitara amehoji ni lini wananchi wanaodai fidia katika maeneo ya Mgodi wa Barrick North Mara Komarera, Nyamichele na Murwambe watalipwa?

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here