Home MICHEZO Msongamano Uwanja wa Mkapa waua mmoja, 30 wajeruhiwa

Msongamano Uwanja wa Mkapa waua mmoja, 30 wajeruhiwa

Google search engine

Na Mwandishi Wetu

Kutokana na hali ya msongamano katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, imeripotiwa kuwa mtu mmoja amepoteza maisha huku wengine 30 wakijeruhiwa.

Hatua ya kutokea kwa msongamano huo umetokana na wingi wa watu waliohudhuria uwanjani hapo kwa ajili ya kutazama mchezo wa fainali ya Kobe la Shirikisho baina ya Yanga dhidi ya USM Alger.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametibitisha kutokea kifo cha mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 na wengine 30 kujeruhiwa.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Mei 28, 2023 na Waziri Ummy kupitia mitandao yake ya kijamii imesema katika hali iliyotokea Uwanja wa Mkapa baada ya mashabiki kusongamana nje ya mageti na mengine kuvunjwa na mashabiki kuingia kwa nguvu uwanjani.

“Taarifa ya Awali: Kuhusu Majeruhi Mkapa Stadium Dar es Salaam. Hadi sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imepokea majeruhi 30 ambapo 1 amefariki (Mwanaume mwenye umri wa takribani miaka 40.

Majeruhi wengi wanaendelea vizuri wana majereha madogomadogo, wanaendelea na vipimo.

Aidha timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ipo uwanjani, inafuatilia kwa karibu kuangalia kama kuna majeruhi wengine,” amesma Ummy.

Katika mchezo huo wa fainali ya kwanza Yanga imepoteza kwa mabao 2-1 huku timu hizo zikitarajiwa kucheza mechi ya marudiano Juni 3, mwaka huu.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here