Home KITAIFA WAZIRI NDALICHAKO ASHIRIKI KIKAO CHA MAWAZIRI KAZI NA AJIRA NCHI ZA SADC

WAZIRI NDALICHAKO ASHIRIKI KIKAO CHA MAWAZIRI KAZI NA AJIRA NCHI ZA SADC

Google search engine

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameshiriki Kikao cha Mawaziri wa Kazi na Ajira wa SADC kilichoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Gilbert F. Houngbo.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 29 Mei, 2023 kwa njia ya mtandao ambapo kupitia kikao hicho wameweza kujadili baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na Bodi ya Magavana wa ILO mnamo mwezi Machi 2023 ambayo yatawasilishwa katika mkutano mkuu wa Shirika la Kazi Duniani utakaofanyika Juni 5 hadi 16, 2023 Geneva, Uswiss.

Masuala yaliyojadiliwa ni programu ya bajeti ya ILO kwa mwaka 2024/2025, hoja ya mabadiliko ya katiba ya ILO ili kuongeza demokrasia katika shirika hilo, ushirikishwaji wa wadau katika uendeshaji wa ILO kwa lengo ya kuongeza haki ya jamii na mapendekezo ya namna ya kuendesha vikao vya ILO vya kikanda.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here