Home KIMATAIFA Zaidi ya watu 100 wafariki baada ya boti iliowabeba watu wa harusi...

Zaidi ya watu 100 wafariki baada ya boti iliowabeba watu wa harusi nchini Nigeria kupinduka

Google search engine

Zaidi ya watu 100 wamekufa maji na wengine hawajulikani walipo baada ya mashua iliyokuwa imewabeba katika mto Niger kusini-magharibi mwa Nigeria kupinduka, mamlaka zimesema.

Meli hiyo ilikuwa imebeba zaidi ya abiria 300 waliokuwa wakisafiri kutoka jimbo la Kwara kuelekea jimbo la Niger baada ya sherehe ya harusi.

Kulingana na maafisa juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea.

Boti hiyo ilipinduka baada ya kuangukia mti, mtawala wa kitamaduni alisema.

“Mamia ya watu wanahofiwa kuuawa na wengine wengi [hawajapatikana]”, taarifa kutoka kwa Gavana wa jimbo la Kwara AbdulRahman AbdulRazaq ilisema Jumanne.

Amiri wa Patigi, Ibrahim Umar Bologi II – mtawala wa jadi wa eneo ambaloajali imetokea – alisema zaidi ya watu 150 wamefariki.

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa mawimbi ya mto yaliifunika boti hiyo na kuilazimu kuangukia mti uliokuwa umesombwa na maji na kusababisha mashua hiyo kupinduka.

Msemaji wa polisi wa jimbo la Kwara ameliambia shirika la habari la AFP kwamba huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka huku juhudi za utafutaji na uokoaji zikiendelea.

Gavana wa jimbo la Kwara Bw AbdulRazaq alitoa “rambi rambi” zake kwa wapendwa wa waathiriwa – na kusema waokoaji walikuwa wakiendelea kutafuta manusura.

Gavana wa jimbo la Kwara Bw AbdulRazaq alitoa “rambi rambi” zake kwa wapendwa wa waathiriwa – na kusema waokoaji walikuwa wakiendelea kutafuta manusura.

Ajali za mtoni katika sehemu hii ya Nigeria ni za kawaida.

Watu wanaoishi katika vijiji vinavyopakana na Mto Niger, ambao unapita katikati mwa nchi, mara nyingi hutumia mto huo kwani unaweza kuwa na kasi zaidi kuliko barabara, ambazo mara nyingi hazitunzwi vizuri na ni hatari kutokana na kuwepo kwa magenge ya utekaji nyara.

Hata hivyo waendeshaji mashua mara nyingi hupakia meli zao zilizochakaa kwa nia ya kupata pesa zaidi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here