Home KITAIFA BILIONI 184 ZIMESHATOLEWA KATIKA HUDUMA ZA UPATIKANAJI WA DAWA

BILIONI 184 ZIMESHATOLEWA KATIKA HUDUMA ZA UPATIKANAJI WA DAWA

Google search engine
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo Juni 16, 2023 kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Wafamasia nchini yaliyofanyika kwa wiki moja Jijini Dodoma.

Na. WAF – Dodoma

Katika mwaka wa fedha 2022/23 jumla ya Shilingi bilioni 184 zimeshatolewa na Serikali kwa ajili ya dawa, haya ni mafanikio makubwa katika Sekta ya Afya nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo Juni 16, 2023 kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Wafamasia nchini yaliyofanyika kwa wiki moja Jijini Dodoma.

“Kipekee namshukuru sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyotoa kipaumbele kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa ambapo ametupatia Bil. 184 ambayo ni sawa na 94% Kati ya Bil. 200 ambazo tumezitenga”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema Rais Dkt. Samia ameamua pia kutoa mtaji kwaajili ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ili iweze kujitegemea kwa kujinunulia dawa yenyewe.

“Kwa kweli katika hili tumshukuru sana Mhe. Rais kwa kuamua kutoa mtaji kwa ajili ya MSD ili wajitegemee wenyewe lakini pia nimpongeze sana Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Mavere Tukai mwanzoni nilikua simuelewi alipokua anasema anahitaji mtaji lakini amejenga hoja vizuri na nimemuelewa hadi tukafanikisha kupatikana kwa mtaji huo”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema Serikali ya awamu wa sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele na kufanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwekeza katika miundombinu, ajira kwa watumishi na upatikanaji wa bidhaa za afya huku akisema kunatakiwa kuwe na kurugenzi ya dawa katika Hospitali.

“Tutaangalia muundo wa hospitali zetu, lazima kuwe na Kurugenzi ya tiba, Kurugenzi ya dawa, Kurugenzi ya Uuguzi, maana haiwezekani Wafamasia wa dawa wasiwe na Kurugenzi wengine wawe nayo”. Amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi amesema Wafamasia ndio nguzo bora inayosimamia upatikanaji wa dawa lakini pia ametoa pongezi kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa kufanikisha kupatikana kwa fedha za ununuzi wa Dawa.

“Tunakushuru sana Waziri kwa kuweza kumshawishi hadi kuelewa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na kufanikisha upatikanaji wa fedha za ununuzi wa dawa kwa zaidi ya asilimia 90 ambazo zitakwenda kusaidia wananchi na kurahisha upatikanaji wa dawa katika vituo vyetu”. Amesema Msasi

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here