Home KITAIFA BENKI YA TIB WAUNGA MKONO KAMPENI YA USAFI UBUNGO, WAFANYA USAFI STENDI...

BENKI YA TIB WAUNGA MKONO KAMPENI YA USAFI UBUNGO, WAFANYA USAFI STENDI YA SIMU 2000

Google search engine
Diwani wa Kata ya Sinza, Raphael Awino, akizungumza na wananchi pamoja na wafanyakazi wa Benki ya TIB ambao wameunga mkono kampeni ya usafi kwa Manispaa ya Ubungo leo Juni 18, mkoani Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Benki ya TIB wakifanya usafi katika Stendi ya Simu 2000 Kata ya Sinza, ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya usafi inayoendeshwa na Manispaa ya Ubungo, leo Juni 18, 2023

Na Mwandishi Wetu

-Dar es Salaam

Katika kuhakikisha kampeni ya kuimarisha Usafi katika Manispaa ya Ubungo inaendelea, leo Juni 18, 2023 benki ya TIB imefanya usafi kwa kushirikiana na watumishi wa Manispaa ya Ubungo katika eneo la stendi ya daladala ya Simu 2000 Mawasiliano

Akiongea baada ya kukamilisha usafi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Lilian Mbassy amesema kuwa wameamua kushiriki kufanya usafi katika eneo hilo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika masuala ya usafi na mazingira hasa katika wiki hii ya utumishi wa umma

Aidha Mbassy ameendelea kusema kuwa wao kama Taasisi ya Fedha wataendelea kutoa ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo kwa Manispaa ya Ubungo

Pamoja na usafi huo, pia benki hiyo wamekabidhi kwa Manispaa ya Ubungo vifaa mbalimbali vya usafi ikiwemo Matoroli 2, mafagio 80, Vikusanya usafi 20, Ndoo za Uchafu 12, Reki 20, Gloves 200 na viatu 30

Akiongea baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Voster Mgina ameipongeza benki hiyo kwa kujitoa kwao kwenye masuala ya usafi na pia amewakaribisha kushiriki shughuli nyingine za kijamii katika Manispaa ya Ubungo

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here