Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki shughuli ya Utumishi wa Umma Afrika zilizofanyika Katika Jiji ya Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Sherehe hizo ambazo huzikutanisha nchi zote wananchama wa Jumuiya ya Afrika zilifanyika zikiwa na ujumbe kuwa mafanikio ya ukuzaji Biashara eneo huru la Biashara Afrika ni hitaji la Utumishi wenye Tija kufanikiwa.
Katika mkutano huo ujumbe wa Tanzania ulitolewa na Naibu Waziri Kikwete ambaye alieleza mafanikio yaliyofikiwa na Awamu ya Sita ya Uongozi wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan yakichagizwa na mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji yaliyofanywa katika Utumishi wa Umma.
Akizungumza Naibu Waziri Kikwete alieleza mabadiliko katika mfumo wa utendaji kazi na utambuzi yaani PEPMIS, PIPMIS na HCMIS ni baadhi ya hatua kubwa kuleta uwajibikaji kazini.
Pamoja na hayo miundombinu inayojengwa ikiwemo Great EA Road inaunga Kenya na Tanzania kwenye kusini na Kaskazini mwa Afrika , Uwekezaji Bandari Ya Dar es Salaam,Reli ya Kisasa (SGR), mabadiliko ya Shirika la Ndege -ATC, Ujenzi wa Vituo vya Biashara vya Pamoja Mipakani na Mradi mkubwa wa Umeme ni alama za mabadiliko makubwa yatakayowezesha Biashara kufanyika vzr na kwa kasi katika eneo la Mashariki na Afrika kwa jumla.
Mkutano unaokuja utafanyika Ethiopia, Mwaka 2025.