SIMBA inaendelea kuliweka imara benchi lao la ufundi baada ya kumtangaza Corneille Hategekimana kuwa kocha wa viungo.
Kocha huyo raia wa Rwanda amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake Msimbazi.
“Uongozi wa Simba umefikia makubaliano kumuajiri Corneille Hategekimana (47) amejiunga na Simba akitokea AS Kigali.” Imeeleza taarifa hiyo.
Simba leo imeongeza watu wawili kwenye benchi la ufundi, awali ilimtangaza Daniel Cadena kuwa kocha wa makipa kwa mkataba wa miaka miwili.