Home BIASHARA Waziri Mkuu kuzindua ofisi za TADB Mtwara

Waziri Mkuu kuzindua ofisi za TADB Mtwara

Google search engine

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, leo anatarajiwa kuzindua ofisi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) Kanda ya Kusini ambayo ipo mkoani Mtwara.

Taarifa ambayo imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkoani Mtwara, imesema Majaliwa atawasili mkoani hapa mchana na kuzindua ofisi hizo za TADB zilipo Mjini Mtwara na baadae kuzungumza na wananchi.

Baada ya hapo anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi mkoani Mtwara kwa siku saba kuanzia kesho Julai 7, 2023.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here