Home KITAIFA CCM MKOA WA IRINGA KUKUTANA NA VIONGOZI WA WILAYA NA KATA ILI...

CCM MKOA WA IRINGA KUKUTANA NA VIONGOZI WA WILAYA NA KATA ILI KUWEKA MAMBO SAWA

Google search engine
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yassin

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yassin amesema chama hicho kitakutana na viongozi wa ngazi ya Wilaya na kata mkoani humo ili kuendelea kujiweka sawa.

Yassin amesema hiyo ni kawaida kwa CCM kukutana na kukumbushana wajibu wa kila mmoja kwenye nafasi yake.

“Ni kweli tutakutana na viongozi wa Wilaya zote na kata zote katika Mkoa wetu, tunataka kukumbushana juu ya wajibu wetu,” amesema Yassin wakati akizungumzia jambo hilo.

Mwenyekiti huyo wa CCM wa Mkoa wa Iringa
amesema moja ya wajibu wa viongozi na Wanachama wa CCM ni kuitetea kwa nguvu zote Serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Moja ya jukumu na wajibu wetu ni kuitetea na kuizungumzia vyema Serikali yetu, hatuwezi kukaa kimyaa wakati kuna watu wanawadanganya wananchi na kuwapotosha, hii haikubariki hata kidogo,” amesema Yassin.

Amesema pamoja na mambo mengine watakumbushana wajibu wao katika kuwaeleza wananchi dhamira njema ya Serikali ya CCM, na kuwaasa waache kusikiliza upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu.

“Sisi Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa, tunaamini kwa dhati dhamira ya Serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe Rais Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ni njema sana,” amesisitiza na kuongeza;

“Hivyo ni wajibu wetu Kumuunga mkono Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, ambaye pia ndiye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,”amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here