NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Chana pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Chen Mingjian wakisaini hati ya makabidhiano ya Vifaa vya Michezo leo Julai 10, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Vifaa hivyo ni pamoja na mipira ya Kikapu 600, Miguu 600, Wavu 600 pamoja na Jezi 2634 ambavyo vitasambazwa Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya Programu ya Michezo Mtaa kwa mtaa pamoja na Samia Taifa Cup.