Home KITAIFA TUME HAKI JINAI YAGUSA WAKUU WA MIKOA, WILAYA….

TUME HAKI JINAI YAGUSA WAKUU WA MIKOA, WILAYA….

Google search engine
Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya tume hiyo kwenye hafla iliyofanyika leo Julai 15, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

TUME ya kuboresha mfumo na taasisi za haki jinai nchini imebaini kuwa wakuu wa mikoa na wilaya hujitambulisha kama wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama kinyume na sheria inayowatambua kama wenyeviti wa kamati za usalama.

 Pamoja na hali hiyo pia, imebaini kuwa wakuu hao huambatana na kamati za usalama katika ziara zao hali inayosababisha hofu kwa wananchi na kuwafanya washindwe kufikisha kero zao kwa kuogopa kukamatwa, kuongeza gharama kwa Serikali kutokana na matumizi ya magari na posho wanazolipwa watumishi hao kwenye ziara hizo.

Akisoma taarifa rasmi ya Tume leo Jumamosi Julai 15, 2023 Ikulu Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman amesema Tume imependekeza wakuu wa mikoa na wilaya wasijitambulishe kama wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama.

Amesema badala yake, viongozi hao wajitambulishe kama wenyeviti wa kamati za usalama wanapoongoza vikao vya Baraza la Usalama la Taifa chini ya Sheria ya Baraza la Usalama.

Mwenyekiti huyo amesema mapendekezo ya Tume kwa wakuu wa mkoa na wilaya wanapotekeleza mamlaka ya ukamataji wazingatie matakwa ya kifungu cha 7 na 15 cha Sheria ya Tawala za Mikoa.

“Masharti hayo ni kosa liwe limetendeka mbele ya kiongozi, liwe la jinai ambalo unaweza kushtakiwa, kosa liwe limesababisha uvunjaji wa amani na utulivu. Baada ya hapo mkuu huyo anatakiwa amuandikie hakimu kumueleza sababu, lakini hilo limekuwa halitendeki.

“Mapendekezo yetu kwenye hili kwamba kiongozi yoyote atakayekiuka maagizo inabidi awajibishwe na serikali,” ameeleza Othman.

Tume ya kuboresha mfumo na Taasisi za haki jinai nchini iliundwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuzinduliwa rasmi Januari 31, 2023 na kuanza kazi Februari Mosi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here