Home BIASHARA BENKI YA EXIM YAJIDHATITI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA YENYE UFANISI WA HALI...

BENKI YA EXIM YAJIDHATITI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA YENYE UFANISI WA HALI YA JUU

Google search engine
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki EXIM Shani Kinswaga

Na Mwandishi Wetu

Benki ya Exim itaendelea na dhamira yake ya kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ili kuboresha utoaji huduma kwa wateja katika matawi yake ndani na nje ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Shani Kinswaga, benki hiyo mwanzoni mwa mwaka huu aliboresha mfumo wake na kuweka miundombinu thabiti, hatua inayolenga kuimarisha utendaji wake na kuwapa wateja hali ya juu ya usalama, ufanisi na uvumbuzi.

“Hii inadhihirisha ari yetu katika kubadilika na kuwa zaidi ya taasisi ya benki. Kama benki, tumejitolea kuwekeza katika kuongeza uwezo li wa mifumo yetu ilikutoa huduma bora kwa wateja wetu na jamii inayotuzunguka,” Kinswaga alisema.

Benki ya Exim ilipata faida ya shilingi bilioni 36.6 kabla ya makato ya kodi kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.9 kwa mujibu wa taarifa ya fedha ya benki hiyo.

Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Shani Kinswaga katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana alisema matokeo ya benki hiyo kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza mwaka huu yanadhihirisha dhamira ya benki hiyo ya kufanya kazi kwa ufanisi kufuatia utekelezaji wa mkakati wa benki hiyo kimamilifu ilikunufaisha wadau wote wa benki hiyo ikiwemo jamii kwa ujumla.

Mapato ya benki hiyo yenye matawi nje ya Tanzania kwenye nchi za Comoros, Djibouti na Uganda yaliongezeka kwa asilimia 9.6 hadi kufikia shilingi bilioni 66.2 kwa miezi sita iliyoishia tarehe 30 Juni 2023 ukilinganishwa na shilingi bilioni 60.4 iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Kinswaga alisema mazingira mazuri ya biashara yalichangia katika utendaji mzuri wa kifedha na kiutendaji wa benki katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2023.

“Uthubutu wetu katika kuwekeza katika teknolojia na uvumbuzi ulituwezesha kutoa huduma za kiwango cha kimataifa zinazoendana na matakwa ya wateja wetu. Tutaendelea kuwekeza zaidi kwenye teknolojia ilikuendeleza ukuaji huu ili kuongeza thamani kwa wadau wetu wote,” Aliongeza.

Kinswaga alisema amana za wateja wa benki hiyo kufikia Juni 30, 2023 ziliongezeka kwa asilimia 9.2 hadi shilingi trilioni 1.9 huku mfuko wa wanahisa nao ukiongezeka kwa asilimia 23.9 hadi kufikia shilingi bilioni 291 ukilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Mapato ya benki hiyo Isiyofadhiliwa (NFI) yalikua kwa asilimia 24.8 hadi kufikia shilingi bilioni 45.3 huku ufadhili wa mikopo ukiongezeka kwa asilimia 11.11 hadi kufikia shilingi trilioni 1.3 ukilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Naye Afisa Mkuu Mtendaji wa benki hiyo Jaffari Matundu, alisema benki hiyo ilichukua hatua madhubti kuimarisha utendaji kazi wake kwa kuzingatia usalama, ufanisi, na uvumbuzi katika huduma zao huku benki hiyo ikiboresha miundombinu yake. Mafanikio ya kuvutia yaliyoshuhudiwa katika utendaji wa benki hiyo katika nusu ya kwanza ya mwaka yanatumika kama kichocheo na yanalenga kuiweka benki hiyo katika mstari wa mbele katika sekta ya fedha.

“Tumejidhatiti kuendelea kuimarisha mifumo yetu ilikutimiza azma yetu ya kutoa huduma zisizo na kifani kwa wateja wetu na kuongeza thamani kwa jamii tunayohudumia,” Matundu alisema.

Matundu alisema benki ya Exim katika kipindi cha miezi sita ya kwanza mwaka huu iliendelea kutekeleza mkakati wake wa Uwekezaji wa Kijamii wa Kijamii (CSI) kutokana Na dhamira yake ya kuleta maendeleo endelevu kupitia programu mbalimbali za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) zinazolenga thamani kwa wadau wake ikiwemo jamii ambazo benki inaendesha shughuli zake.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here