Uwepo wa rais wa Urusi katika mazishi ya Yevgeny Prigozhin “haukutarajiwa,” msemaji wa Putin Dmitry Peskov alisema. Kulingana naye, Kremlin haina hata habari kuhusu wakati na mahali pa mazishi.
“Uamuzi juu ya suala hili unafanywa na jamaa na marafiki, hapa hatuwezi kusema chochote bila wao,” Peskov alinukuliwa akisema na mashirika ya habari ya Urusi.
Mkuu wa Wagner PMC, alifariki katika ajali ya ndege ya kibinafsi katika mkoa wa Tver mnamo Agosti 23, na alikuwa kwenye orodha ya abiria, na siku chache baadaye Kamati ya Uchunguzi ilitangaza kutambua mabaki ya mwili wake. Jumla ya watu 10 walifariki katika ajali hiyo.
Mnamo Agosti 24, Putin alisema kwamba alikuwa amemfahamu Prigozhin (akimzungumzia katika wakati uliopita, ingawa wakati huo kifo cha kiongozi huyo wa Wagner hakikuwa kithibitishwa rasmi) tangu mwanzoni mwa miaka ya 90, jambo ambalo liliwashangaza watafiti wenye uzoefu wa uhusiano wao, ambao waliamini kuwa urafiki waoulianza labda baadaye.
Putin aliliita Kundi la Wagner kuwa ni kundi la usaliti wa Urusi, lakini haikumzuia kukutana na kiongozi wake baada ya matukio yaliyodaiwa kuwa ya usaliti angalau mara moja, na labda hata mara mbili.
CHANZO: BBC