Home KITAIFA RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI LA SKULI YA MILIONI 600/- INAYOJENGWA...

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI LA SKULI YA MILIONI 600/- INAYOJENGWA NA NMB

Google search engine
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu (watatu kulia) Hassan akiweka jiwe la msingi aliloweka kwenye ujenzi wa Skuli ya maandalizi ya Tasani alipotembelea eneo hilo ambapo skuli hiyo itajengwa na Benki ya NMB na kukamilika mwezi wa kumi na mbili na kuanza kupokea wanafunzi mwezi January mwakani. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna Wapili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipokea maelezo ya ujenzi wa Skuli ya maandalizi ya Tasani kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wapili kushoto) alipotembelea eneo la Tasani na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa skuli hiyo ya maandalizi ambayo ujenzi wote na uwekaji wa samani utagharamiwa na Benki ya NMB. Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid na kushoto ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipokea maelezo ya ujenzi wa Skuli ya maandalizi ya Tasani kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wapili kushoto) alipotembelea eneo la Tasani na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa skuli hiyo ya maandalizi ambayo ujenzi wote na uwekaji wa samani utagharamiwa na Benki ya NMB. Wapili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid, wapili kushoto ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na kushoto ni Meneja wa Biashara wa Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Said Shaame.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan (wapili kulia) akipokea maelezo ya ujenzi wa Skuli ya maandalizi ya Tasani kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wapili kushoto) alipotembelea eneo la Tasani na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa skuli hiyo ya maandalizi ambayo ujenzi wote na uwekaji wa samani utagharamiwa na Benki ya NMB. Watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid, wapili kushoto ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na kushoto ni meneja wa Biashara wa Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Said Shaame na kulia ni Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali wa Zanzibar, Lela Mohamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipokea maelezo ya ujenzi wa Skuli ya maandalizi ya Tasani kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wapili kushoto) alipotembelea eneo la Tasani na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa skuli hiyo ya maandalizi ambayo ujenzi wote na uwekaji wa samani utagharamiwa na Benki ya NMB. Wapili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid, wapili kushoto ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na kushoto ni meneja wa Biashara wa Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Said Shaame.

NA MWANDISHI WETU

-ZANZIBAR

KUELEKEA kilele cha Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2023), linaloendelea Paje, Mkoa wa Kusini Unguja, visiwani Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Samia Suluhu Hasaan, ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Skuli ya Maandalizi Tasani, iliyopo Sheia ya Tasani, Makunduchi, inayojengwa na Benki ya NMB, ikitarajia kugharimu Sh. Milioni 600 hadi itakapokamilika Desemba 2023.

Tamasha la Kizimkazi linaloambatana na Maonesho ya Bidhaa mbalimbali, likifanyika chini ya kaulimbiu ‘Tuwalinde Kimaadili Watoto Wetu kwa Maslahi ya Taifa,’ lilizinduliwa na Rais wa Zanzibar na Dk. Hussein Ali Mwinyi, Agosti 26 na litafungwa na Rais Samia, Alhamis ya Agosti 31, ambapo pamoja na mambo mengine linatumika kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na wadau zikiwemo taasisi binafsi.

Akitoa maelezo ya awali ya mradi huo kwa Rais Samia, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB (CEO), Ruth Zaipuna, alisema ujenzi huo ambao ni sehemu ya Programu ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI), ni kati ya jitihada za wazi za benki yake katika kumuunga mkono kufanikisha Sera ya Elimu Bure kwa Shule za Msingi hadi Sekondari nchini, hasa ikizingatiwa kuwa Elimu ni Msingi Imara na Muhimu kwa Maendeleo ya Taifa.

Bi Zaipuna alimueleza Dk. Samia kwamba ujenzi huo utakaojumuisha madarasa matano yatakayochukua wanafunzi 200 kwa mkupuo mmoja, utakamilika Desemba mwaka huu, tayari kabisa kwa Mwaka wa Masomo wa 2024, ambao utaanza Januari mwakani, na kwamba Skuli ya Maandalizi Tasani itakuwa ni shule ya kwanza katika eneo hilo, ikiwa ni ya tatu kwa mji wa Makunduchi.

“Ujenzi wa majengo na samani za ndani kama vile viti, meza na madawati, utaigharimu Benki ya NMB Shilingi Milioni 600, ambazo ni sehemu ya faida yetu tunayoitoa kila mwaka kurejesha kwa jamii. 

“Mradi huu ulio kwenye eneo la mita za mraba 467, utajumuisha madarasa matano yatakayobeba wanafunzi 40 kila moja, Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Ofisi ya Walimu, jiko, vyoo vya walimu, wafanyakazi na wanafunzi, stoo, Mifumo ya Kisasa ya Maji Safi na Majitaka, pamoja na sehemu ya michezo.

“Mheshimiwa Rais, mradi wa Skuli hii ni uthibitisho wa utayari wa NMB kusapoti Serikali ya Tanzania katika juhudi zake za kuboresha Elimu nchini. 

“Tunatambua jitihada zako katika Sekta ya Elimu, nasi tukiwa wadau na washirika muhimu, tukaona ni vema kuunga mkono maono yako ya Elimu Bora. NMB tunajivunia kuwa washirika vinara wa hilo, tukiamini Skuli ya Maandalizi Tasani inaweza kuibua wasomi watakaokuja kuwa viongozi wakubwa,” alibainisha CEO Zaipuna.

Akizungumza baada ya maelezo hayo, Rais Samia aliishukuru Benki ya NMB kwa namna inavyounga mkono jitihada za Serikali yake na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika kuboresha Mazingira ya watoto kupata Elimu, huku akiweka ahadi ya kurudi Tasani Januari mwakani wakati wa kuzindua shule hiyo.

“Tunaishukuru sana sana Benki ya NMB kwa kuamua kutuunga mkono kwa kufanya hili la Ujenzi wa Skuli hii kwa ajili ya watoto wetu. Nilikuwa hapa mwaka jana kuzindua Ofisi ya Sheia, Niko hapa kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi huu na utakapokamilika, nitarudi Januari mwakani kuja kuizindua.

“Niwakumbushe Wana Tasani kwamba niliwaahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali na huu ndio muendelezo wa hilo. Sisi ni viongozi wenu, na sio watawala wenu. Tuko kazini kila uchao kutatua kero zenu, jukumu lenu ni kushirikiana na Serikali kwa kuwasililiza viongozi wa ngazi mbalimbali na kuacha maneno maneno. NMB watapokamilisha, yatunzeni majengo haya muhimu kwa elimu za watoto wetu,” alimalizia Rais Samia.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here