Na Mwandishi Wetu
-NJOMBE
WIZARA ya Utamaduni Sanaa na Michezo imesema kupitia maboresho makubwa yanayokwenda kufanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Benjamini Mkapa mkoani Dar es Salaam, Serikali inakwenda pia kuweka mfumo wa Intanet bure ili kuwawezesha mashabiki kupata huduma hiyo wawapo ndani ya uwanja huo.
Hayo yamesemwa mjini Njombe na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu wakati akifungua kikao kazi cha 14 kwa maafisa maendeleo utamaduni na maofisa maendeleo ya michezo wa mikoa upande wa Tanzania Bara.
“Tunakwenda kushirikiana na wenzetu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo watatuwekea mfumo wa WiFi ya bure utakuwa ukiingia uwanjani kuangalia mpira lakini pia utakuwa unapata Free WiFi itakuwepo pale,” amesema Yakubu. Katika mkutano huo, katibu amegawa mipira 54 kila mkoa ambapo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Ally Mayai amesema mipira hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Samia Taifa CUP yatakayofanyika Oktoba mwaka huu