Home KITAIFA MRADI WA BBT UMETOA FURSA YA AJIRA KWA VIJANA,AKABIDHIWA TUZO YA UZALISHAJI...

MRADI WA BBT UMETOA FURSA YA AJIRA KWA VIJANA,AKABIDHIWA TUZO YA UZALISHAJI MBEGU BORA

Google search engine
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Vyakula Duniani, Jakaya Mrisho Kikwete katika aliyeshika tuzo akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mbegu bora na kilimo katika mkutano wa pembeni wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika Septemba 5-8, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Vyakula Duniani, Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa kumtangaza mshindi wa tuzo ya uzalishaji mbegu bora leo Septemba 07, 2023  katika mkutano wa pembeni wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika Septemba 5-8, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) 
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano wa pembeni wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika Septemba 5-8, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) 

NA MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

MRADI wa Jenga kesho iliyo Bora, (Better Building Tomorrow (BBT) umetoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana na wanawake kuliko sekta nyingine, pia umejenga ushawishi wa vijana wengi kuingia kwenye kilimo.

Hayo ameyasema hayo leo Septemba 7, 2023 na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Vyakula Duniani, Jakaya Mrisho Kikwete katika mkutano wa pembeni wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) linaloendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo Rais Kikwete, amesema mradi huo ni mhimu hapa nchini kwani umechukua idadi kubwa ya watu.

Katika mkutano huo pia Dkt. Kikwete amemkabidhi tuzo yenye thamani ya million 250 kwa mshindi wa kwanza ambaye alizalisha mbegu bora Afrika.

Tuzo hiyo imenyakuliwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Pan Afrika ya Utafiti wa Maharage, Jean Rubyogo ambaye alifanya kazi ya kuzalisha mbegu bora kwaajili ya kuendleza Kilimo barani Afrika na tuzo hiyo imesimamiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Mifumo ya Chakula (AGRA).

Akizungumzia kuhusiana na mashindano ya kuzalisha mbegu bora,Kikwete amesema kuwa mashindano yalianza Mei Mwaka huu na mapendekezo yalikuwa 101 na baadae walisogeza muda na yafikia mapendekezo 496, baada ya hapo kamati ikakaa na kuchambua mapendekezo hayo na kufikia 19 na wakaendelea na kuchambua mpaka akapatikana mshindi.

“Wataalamu kutoka AGRA na wengine walichambua mapendekezo haya walipata 19 yakaletwa kwenye kamati yetu kufanya uchambuzi yakabaki mawili tuliunda kamati ndogo kufanya uchambuzi wa hayo mawili hadi kupata mshindi wa leo,” amesema Kikwete.

Amesema taasisi iliyochukua tuzo imefanya utafiti wa maendeleo ya mbegu ya maharage aina 650 mbegu zinazo himili changamoto mbalimbali za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi, kama joto, kuhimili magonjwa na wadudu na maharagwe yake yana madini ya Zinc na chuma.

Aidha amesema mshindi huyo atakabidhiwa tuzo leo jioni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here