Home KITAIFA DC KASILDA AWATAKA WAFUGAJI SAME KUFUGA KISASA

DC KASILDA AWATAKA WAFUGAJI SAME KUFUGA KISASA

Google search engine
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni, akizungumza na wakati wa uzinduzi wa mnada wa mifugo na mazao leo Septemba 13, 2023

NA ASHRACK MIRAJI

-SAME

Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewataka wafugaji wa asili wilayani hapa kuhakikisha wanafuga kisasa na kuacha kufuga kimazoea ili kuepuka athari zinazotokana na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo mifugo mingi hufa Kwa kukosa malisho.

Hayo ameyasema leo Septemba 13, 2023 wakati wa ufunguzi wa soko jipya la mnada wa ng’ombe na mazao mbalimbali ya chakula huku lengo likiwa kukuza uchumi wa wilaya na wafugaji hao kuuza mifugo kabla ya kipindi cha ukame kuanza ni muda muafaka sasa wafugaji hao kutumia Soko jipya la Mnada Kirinjiko lililopo wilayani humo kwa kuuzia mifugo yao.

DC Kasilda, amesema Serikali imewawekea mazingira mazuri ikiwemo miundo mbinu ya kisasa kwa ajili ya Kuendesha mnada katika eneo hilo.

“Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwakuelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya Maendeleo ikiwemo kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, afya, elimu pamoja na miundombinu ya barabara na maji,” amesema DC Mgeni

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Same, Anastasia Tutuba amesema mpaka sasa kwenye eneo hilo halmashauri imeshapima vizimba zaidi ya 600 na kwamba kama halmashauri wataendelea kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana katika eneo hilo lengo likiwa ni kuiongeza mapato na kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here