Home KITAIFA AICC YAELEZA MIKAKATI KUVUTIA MIKUTANO KIMATAIFA

AICC YAELEZA MIKAKATI KUVUTIA MIKUTANO KIMATAIFA

Google search engine

MAFURU AZIMULIKA TAASISI ZINAZODAIWA ZAIDI YA BILIONI 7/-, WADAIWA KUFIKISHWA KWA MSAJILI HAZINA

Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Ephraim Mafuru, akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu shughuli za taasisi yake
Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Ephraim Mafuru
Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Ephraim Mafuru, akizungumza na wahariri leo Septemba 14, 2023 Jijini Dar e s Salaam
Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri akifafanua baadhi ya mambo katika mkutano
Baadhi ya Wahariri wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Ephraim Mafuru leo Septemba 14, 2023 Jijini Dar es Salaam

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

KITUO cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kimejipanga kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu bora Afrika katika kupokea watalii wa mikutano kutoka nafasi ya tano kwa sasa.

Kutokana na hatua hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Ephraim Mafuru, anasema kuwa utajiri wa miaka wa 45 ya historia ya AICC pamoja na wito wake; We Bring the World to Tanzania (Tunaileta Dunia Tanzania), unakwenda kudhihirishwa na mkakati wake kwa kuhakikisha wanaandaa mikutamo ya kimataifa ambayo imekuwa ikiitangaza Tanzania katika ramani ya dunia.

Akizungumza leo Septemba 14, 2023 Jijini Dar es Salaam katika mkutano ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari, Mafuru, amesema kuwa kwa mujibu wa Chama cha Kimataifa Vituo vya Kimataifa vya Mikutano Duniani (ICCA), Tanzania ipo nafasi ya tano katika idadi ya watalii wa mikutano ya kimataifa Afrika ambayo ni asilimia 10 ya soko la mikutano yote ya kimataifa inayofanyika Afrika.

Mafuru amesema kuwa ili kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika medani za utalii wa mkutano Afrika, AICC imedhamiria kuboresha miundombinu yake kwa kumbi za kisasa za mikutano ya kimataifa, hoteli za hadhi ya nyota tano, maduka makubwa, benki pamoja na viwanja vya michezo na burudani jijini Arusha sambamba na katika Jiji la Dar es Salaam ambapo pia wanaendesha Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere zmbao ni ukumbi wa kisasa chenye nafasi kwa mikutano hadi wajumbe 1003. Kwa jumla kuna vyumba na kumbi za mikutano 12.

“Kiutawala kituo hiki ni tawi la AICC (Arusha International Conference Center). Tumedhamiria kujenga mji wa kisasa katika eneo la ekari 90.8 na kuipaisha Tanzania na jiji la Arusha kuwa siyo tu kuwa sehemu maarufu kwa utalii wa Mikutano bali pia nchi ya kila aina ya michezo na burudani,” amesema.

Mafuru amesema AICC itajenga kituo cha Kimataifa cha Mikutano kitakachojulikana kama “Kituo cha kimataifa cha Mikutano Kilimanjaro” katika eneo hilohilo lilipo eneo la D1 na E lilipo kijenge unapoelekea barabara ya Njiro.

Pamoja na hilo pia ameeleza mpango mwingine wa kujenga mji mwingine wa Kisasa utakaohusisha kituo cha Kimataifa cha mikutano, benki, viwanja vya michezo na maduka makubwa katika jiji la Zanzibar na baadaye Dodoma.

“Kituo hiki kinamilikiwa kikamilifu na Serikali na kinafanya kazi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo kinatoa taarifa Bungeni.

“AICC ilianzishwa ili kusimamia na kudhibiti Kiwanja cha Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyokufa na majengo na ardhi nyingine zote katika Jiji la Arusha ambazo zilikuwa mali ya Jumuiya iliyokufa na kutoa vifaa na huduma kwenye kiwanja hicho kwa madhumuni ya makongamano, mikutano, semina na kadhalika.

“Na kwamba kama halmashauri wataendelea kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana katika eneo hilo lengo likiwa ni kuiongeza mapato na kuinua uchumi wa wananchi wa Arusha na Dar es Salaam. AICC inafanya kazi kama huluki za kibiashara bila ruzuku ya Serikali kwa lugha nyepesi tunajiendesha wenyewe.

“Yapo maeneo kadhaa ya kibiashara ya kituo hiki ni pamoja na huduma za za mikutano, kukuza Utalii wa Biashara,  Ofisi na vitengo vya makazi kwa kukodisha na utoaji wa huduma za hospitali katika hospitali yetu ya AICC iliyopo Jijini Arusha ambayo inahudumia wagonjwa zaidi ya 7000 kwa mwezi,” amesema Mafuru

Mkurugenzi huyo amesema kuwa amesema kuwa watanedelea kusimamia dira yao ya kuwa mfano na kuwezesha utalii wa biashara pamoja na kukuza na kutoa huduma bora za utalii wa biashara kwa wateja wa kitaifa na kimataifa kwa maendeleo ya kitaifa, kijamii na kiuchumi.

UKUMBI WA SIMBA

Akieleza ukumbi wa kumbi zao na huduma wanazotoa Mfarufu, amesema kuwa katika Ukumbi wa Simba unabeba viti 1,350 ikiwamo kufunga Televisheni kubwa na ukuzaji sauti wa kitaalamu.

UKUMBI WA ZIWA NYASA

Amesema ukumbi huo una vifaa vya matumizi vinavyobadilika kuendana na matumizi tofauti, mpangilio na muundo wa ukumbi kama eneo la usajili, eneo la kuhifadhia muda, sehemu za kupakia na kupakua, jiko la kisasa na mgahawa.

HATIMA ILIYOTIMIA

Mbali hilo pia huuma mbalimbali wamejitahidi kuimarisha kwa kushrikiana na wadau pamoja na mamlaka za Serikali ikiwamo Halmashauri ya Jiji la Arusha ikiwamo mbali ya kuwa na makazi na huduma za kumbi kwa kujenga mazingira salama na rafiki  ikiwamo huduma za kibenki, maduka ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) pamoja na kuwa na huduma nzuri ikiwamo za matibabu katika Hospitali ya AICC.

NAMNA YA KUFIKA KUTOKA ARUSHA

Mafuru amesema kuwa katika kuhakikisha Kituo hicho cha Mikutano cha Kimataifa kinatoam huduma bora ni rahisi kufika kwa wageni ambao wamekuwea wakitumia usafiri wa ndege za kimataifa za mashirika ya Ethiopian Airlines,   Qatar Airways, Rwanda Air, KLM, Eurowings Discover, Air Uganda, KQ, Charter Flights

UENDESHAJI HOSPITALI

Mkuruegenzi huyo amesema kuwa AICC inaendesha hospitali ya ukubwa wa kati ya vitanda 32 yenye vifaa vya uchunguzi vya maabara vya kompyuta, ambavyo ni pamoja na, miongoni mwa vingine, mashine ya kisasa ya X-ray, kiti cha Meno kilichounganishwa pamoja na mashine ya sauti ya juu zaidi na kliniki ya tiba ya mwili.

“Hospitali hii inahudumia wakazi wa Arusha na wajumbe wa mikutano, baadhi kutoka UN, EAC, wafanyakazi wa AU, watalii, wafanyabiashara pamoja na wateja wa ndani.

“Mwenyeji wa ICTR makubaliano ya Arusha kwa Rwanda (pia yanajulikana kama Makubaliano ya Amani ya Arusha, au mazungumzo ya Arusha) yaliwekwa na kutiwa saini katika AICC huko Arusha, Tanzania mnamo Agosti 4, 1993, na Serikali ya Rwanda na waasi wa Rwandan Patriotic Front (RPF), chini ya uongozi wa Serikali ya Rwanda. upatanishi, kumaliza Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitatu vya Rwanda,” anasema

ATHARI ZA KIUCHUMI ZA MATUKIO YA BIASHARA

Kutokana na Sekta ya Baraza la Matukio, (2019) inaelezwa kuwa jumla  ya Athari za matukio ya biashara ya Kimataifa milioni 27.5 ajira zinazoendelezwa na matukio ya biashara ya Global

USHIRIKIANO WA AICC/JNICC

Moja ya kati ya mkakati wa kituo hicho ni kuongeza ushirikiano na wadau muhimu kwa mfano kama TTB, Shirika la Ndege la Air Tanzania, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (Authorities Airport), watoa huduma za watalii, wenye mahoteli, wafanyabishara balozi za nje, TANAPA, Ngorongoro Conservation, NHC na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

UENDELEZAJI UPYA WA VIWANJA/MALI ZILIZOPO

“Mradi wa upanuzi wa Hospitali ya AICC – wa muda wa kati Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mlima Kilimanjaro (MK-ICC) – Muda wa mrefu na wa kati.  Ukarabati na upanuzi wa JNICC

CHANGAMOTO

Mafuru amesema pamoja na uwepo wa mafanikio lakini bado wamekuwa wakikabilina na changamoto kadhaa ikiwamo baadhi ya taasisi zilizopewa huduma kushindwa kulipa madeni yake licha ya kupewa huduma na kituo hicho.

“Kwanza ni lazima tuseme itafika wakati tutaomba kibali cha Msajili wa Hazina kwamba ili tukuruhusu kutumia kumbi zetu kwa taasisi ni lazima ulipe kabisa. Kwa maana sasa una madeni ambayo tunadai yanafikia kiasi cga Shilingi Bilioni 7.

“Tuna unakuta hito taasisi imejitangazia kuingiza faida lakini kwa hali ilivyo tutaomba kibali kabla ya kusoma faida za hesabu zako kwanza lipa deni letu badala ya kusoma jumlajumla. Ninaamini ushirikiano wetu Wahariri utakwenda kuamsha watu hao kutambua kuwa wanadaiwa,” amesema Mafuru

“Jumla ya deni ni Shilingi Bilioni 7.4 kati ya hao wadaiwa 17 hadi 20 ni Taasisi za Serikali ambapo ni sawa na asilimia 65  ya deni lote  ambalo ni sawa  na Shilingi Bilioni 4.76zinazodaiwa na Taasisi za Serikali.

“…. timu za bodi na wasimamizi kupata kufichua maeneo yenye utendaji bora na vituo vya mikusanyiko ili kupata ujuzi wa sekta.

AICC itashawishi Msajili wa Hazina ili utendaji wa watendaji wakuu upimwe jinsi wanavyolipa madeni ya ndani,” amesema

MTARAJIO

Mafuru amesema kutokana na hali hiyo bado wamekuwa na matarajio ndani ya AICC ikiwamo kuandaa mikutano 30 ya kimataifa kwa mwaka, iliyohudhuria wastani wa watu 1000, wakitumia wastani wa USD 400 kwa siku katika siku 4, hii itatafsiri kuwa USD 48m ya mapato.

“Kwa kuongeza idadi hii ya wajumbe hadi 2000, mapato haya yatakuwa USD 96m kwa mwaka. Kama nchi tunahitaji kuunganisha juhudi zetu za kuiweka upya Tanzania kama kimbilio la mwisho la mkutano barani huku kukiwa na ahadi ya pamoja na isiyo na masharti iliyobaki,” amesema Mkurugenzi huyo wa AICC

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here